Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndo hivyo, Everton kuuza mastaa wote

Evertonnn Ndo hivyo, Everton kuuza mastaa wote

Sat, 1 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Everton imethibitisha kwamba mpango wa kuiuza klabu hiyo kwa kampuni ya 777 Partners umekwama na hautakuwapo tena.

Kinachoelezwa ni kwamba Everton sasa ipo kwenye hatari ya kuwekwa chini ya mamlaka za Ligi Kuu England endapo kama tajiri waKE, Farhad Moshiri atashindwa kupata mtu mwingine wa kumuuzia timu hiyo yenye maskani yake Goodison Park.

777 Partners’ ilikuwa na mpango wa kuinunua timu hiyo kwa Pauni 500 milioni huku Pauni 200 milioni tayari zilikuwa zimewekezwa kwenye klabu.

Lakini, mabosi wa Ligi Kuu England wamegoma kuidhinisha mchakato huo baada ya kampuni hiyo yenye maskani yake Miami, Marekani, kutokuwa na pesa za kutosha baada ya wakala wa bima wa Marekani, A-Cap kujiondoa. Kampuni hiyo pia inakabiliwa na masuala la kisheria Marekani na Ulaya.

Ukata wa kifedha uliifanya Everton kupokwa pointi msimu uliopita, lakini ilipambana na kunusurika kushuka daraja. Na sasa kama itakuwa chini ya mamlaka, basi itakatwa pointi tisa msimu ujao.

Klabu hiyo kwa sasa ina deni linaloripotiwa kufikia Pauni 583 milioni. Kutokana na hilo, kila mchezaji wa Everton kwa sasa yupo sokoni ili kupata pesa ya kufanya timu kujiiendesha.

Mwisho wa mwaka wa fedha kwa klabu hiyo ni Juni 30, hivyo baada ya hapo tajiri Moshiri atakuwa na siku 16 tu za kuuza wachezaji ili kuweka sawa vitabu vyake vya hesabu.

Chanzo: Mwanaspoti