Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndemla, Banda waamsha shangwe

Wasili Pic Ndemla, Banda waamsha shangwe

Sat, 22 Jan 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Mtibwa Sugar nayo ina mastaa wao,ukitaka kuamini hilo,baada ya basi kutua uwanjani (Manungu), wapo walioongoza kwa kushangiliwa zaidi.

Mtibwa Sugar inacheza dhidi ya Simba saa 10:00 jioni, baada ya wachezaji wao kushuka, wapo walioshangiliwa zaidi na kupewa maagizo ya kufanya.

SAID NDEMLA Jina la kiungo wa timu hiyo,Said Ndemla lilitajwa zaidi huku wakimpajika jina la Mzee wa Mashuti na kumwambia wanamtegemea aisaidie timu.

ABDI BANDA Beki wa timu hiyo,Abdi Banda alishangiliwa zaidi na ameambiwa wanacheza nyumbani aibebe timu.

RASHID BABA UBAYA Wakati anashuka alipokewa na shangwe, huku wakimwambia ni mtoto wa nyumbani,hivyo asiwaangushe.

Ukiachana na hao, mashabiki wa timu hiyo, walikuwa wanalitamka jina la Deo Kanda kwamba wanaamini uzoefu wake utaibeba timu.

Chanzo: Mwanaspoti