Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndayiragije: Tupo salama Cameroon

D4581b70ff9c12b429a59d1fd2c80acd Ndayiragije: Tupo salama Cameroon

Sun, 17 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KOCHA Mkuu wa Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Ettiene Ndayiragije amesema mlipuko uliotokea nje ya Uwanja wa Limbe, Cameroon hauwezi kuathiri malengo yake kwenye Mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Chan) kwa sababu amewaandaa wachezaji wake kisaikolojia.

Milipuko iliripotiwa nje ya Uwanja wa Limbe Omnisport Alhamisi iliyopita kuelekea kwenye mashindano hayo na Cameroon imekabiliwa na ukosoaji kwa kutumia uwanja wa mwenyeji wa mkoa wa Kusini-Magharibi wakati hali ya utulivu wa ndani ni mdogo.

Timu za Kundi D ambazo ni Tanzania, Zambia, Guinea na Namibia zinatarajiwa kucheza kwenye Uwanja huo na Tanzania inatarajiwa kucheza na Zambia Jumanne ijayo mchezo utakaochezwa saa 1:00 usiku

Licha ya hali hiyo huko Limbe, Kocha wa Taifa Stars, Ndayiragije amesema kuwa hawajaathiriwa wala hawajasumbuliwa tangu walipofika mjini hapo na wanajiandaa kucheza mechi yao ya ufunguzi bila kufikiria kile kinachotokea.

"Tumehakikishiwa kuwa kuna usalama, na hatujaathiriwa na chochote tangu tumefika hapa, lengo letu lipo kwenye kile kilichotuleta, kucheza kwenye mashindano, na tayari tumeweka malengo yetu na nguvu zetu kwenye mashindano tu,” alisema Ndayiragije.

"Tumewaomba wachezaji wasiwe na wasiwasi juu ya hali hiyo, tuko hapa kucheza na kushinda mechi zetu na hiyo ndiyo lengo letu kuu hapa,"

Shambulio hilo halikuwa na vifo ila magari kadhaa yaliharibiwa huku kukiwa na wasiwasi unaoendelea juu ya usalama wa mkoa huo kwa sababu ya mvutano wa kujitenga.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo dhidi ya Zambia alisema wachezaji wote wako salama isipokuwa mshambuliaji John Bocco kwani hajapokea taarifa kutoka kwa madaktari ikiwa ataweza kuanza dhidi ya Chipolopolo.

"Sijapokea habari zozote kuhusu Bocco, bado yuko chini ya uangalizi wa madaktari na hawajanipa ripoti hivyo sijui kama atakuwa fiti kucheza kwenye mechi hiyo,”.

Bocco, nahodha wa Taifa Stars na Simba, alipata majeraha katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum ambao walishinda kwa mabao 4-0.

“Ni jukumu letu kuwaelekeza wachezaji tunachotakiwa kufanya, hatujali wapinzani wetu wamejiandaaje au wakoje sijui, tunachoangalia kwetu ni kupambana na kuibuka na ushindi na hili ndio lengo letu,”alisema.

Tanzania mara ya mwisho kucheza na Zambia ilikuwa kwenye mashindano ya COSAFA ambapo ilipoteza kwa mabao 4-2.

Baada ya mchezo huo Stars itakutana na Namibia Januari 23, mwaka huu na itamaliza mchezo wa mwisho dhidi ya Guinea, Januari 27.

Jumla ya wachezaji 27 wapo Cameroon kupeperusha vyema bedera ya Taifa hivyo, macho ya Watanzania wote yamewaelekea wao.

Wachezaji waliopo Cameroon ni Aishi Manula, Juma Kaseja, Dan Mgore, Shomari Kapombe, Israel Mwenda, Edward Manyama, Yassin Mustapha, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Ame, Carlos Protas, Said Ndemla, Baraka Majogoro, Zuberi Dabi na Yusuph Mhilu.

Wengine ni Ayoub Lyanga, Feisal Salum, Rajabu Athuman, Ditram Nchimbi, John Bocco, Deus Kaseke, Lucas Kikoti, Farid Mussa, Adam Adam, , Abdulrazack Hamza, Khelfinnie Salum, Samwel Jakson, Omari Omari na Paschal Gaudence.

Mashindano hayo yalianza jana kwa wenyeji Cameroon kucheza na Zimbabwe Uwanja wa Ahmadou Ahidjo- Yaoundé ssa 10:00 jioni.

Mataifa 16 yataoneshana uwezo wa kusakata kandanda katika makundi manne yenye timu nne kila moja.

Chanzo: habarileo.co.tz