Mchezaji wa Ubelgiji ambaye wazazi wake wanatoka Burundi na Rwanda, alishinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika katika ligi ya soka ya Ubelgiji.
Mike Trésor Ndayimimiye mwenye umri wa miaka 23 alitunukiwa tuzo ya Soulier d'ébène Jumatatu usiku, baada ya kutimiza ahadi yake ya kutoa mipira zaidi (pasi) kutokana na mashambulizi (23) na kufunga mashambulizi manane katika michezo 37 hadi sasa.
Mike Trésor, anayeichezea klabu ya Genk, pia ameichezea timu ya taifa ya Ubelgiji ya walio chini ya miaka 16 na 21, lakini bado hajachezea kwenye timu ya taifa ya 'Diables Rouges'.
Baba wa kijana huyu ni Freddy Ndayishimiye aliyewahi kucheza na na pia kama nahodha wa timu ya taifa ya Burundi na mama yake mzazi ni Mnyarwanda, katika ukurasa wake wa Instagram anaonyesha bendera za Burundi na Rwanda zikiwa ni nchi anazotoka.
Baada ya kushinda tuzo hii, alipoulizwa kuhusu hisia zake, alisema: “Nina furaha kutuzwa. Ninajivunia kuwakilisha familia yangu na nchi zangu.”
Alipoulizwa siri yake ya kupasisha mipira vizuri, alisema: “Sidhani kama kuna siri nyingine, naweza kusema huenda ilitokana na zawadi ya familia kwa sababu baba naye alikuwa na mkono mzuri sana, ingawaje sichezi kutumia mkono wa kushoto lakini lishe yangu pia ni nzuri sana."
Katika hafla ya kupokea tuzo hii aliulizwa iwapo angependa kuichezea timu ya taifa ya Ubelgiji na kufuata nyayo za wachezaji wengine wa Kiafrika kama Emile Mpenza, Romelu Lukaku, Vincent Kompany, Marouane Fellaini na pia kuichezea timu ya taifa ya Ubelgiji 'Diables Rouges'.
Alijibu: “Ndiyo sana, ninajaribu kufanya kazi kwa bidii ili kupata nafasi yangu lakini [kuna] watoa maamuzi. Nitaendelea kufanya kila niwezalo na tutaona itatufikisha wapi."