Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndani ya Simba SC kuna kelele mbili - Farhan

Mangungu Mo Dewji Mo Dewji na Mangungu

Thu, 11 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ndani ya hii timu yangu SIMBA kuna kelele mbili ambazo zote zina mashiko nami nahitaji muda kutulia kufanya tafiti na kufahamu ukweli upo wapi kwakuwa Uandishi sio suala la kuwahi kupost bali kupost taarifa sahihi hata kama kwa kuchelewa.

Kelele ya kwanza ni kuwa timu imekwama kimuundo kwa maana Viongozi waliopo wameshindwa kuisukuma timu mbele, timu imeganda sehemu moja, CEO Kajula kila press ni mambo ya biashara pekee na ana muda hajaongea chochote kuhusu football development.

Kelele hii inaenda mbali na kuhoji kuwa Simba ina kamati ya usajili? Kama ipo wapo wakina nani? Simba ina Scout? Jibu ni ndio je Scout anaripoti kwa nani? Jibu ni Mkurugenzj wa Ufundi, je yupo? Anafanya kazi yake? Kama vyote hakuna je nani Mhusika Mkuu wa sajili zote?

Kelele hii inaulizia pia ipo wapi Kamati ya Mashindano? Kama ipo wapo wakina nani? Kama hakuna ina maana timu ipo chini ya Watu wawili pekee? Kwa maana ya Mwenyekiti Salim na CEO pekee? Wapo wapi Viongozi wa zamani wa timu? Wapo mbali sana na timu, ni kwanini? Kipi kimefichika?

Kelele ya pili inasema MO DEWJI hatoi mzigo kwenye timu (japo hii nina mashaka nayo sana) ndio maana timu haifanyi vizuri zikitajwa bonus ni changamoto na kelele hii imeenda mbali zaidi na kudai kuwa nje na Wadhamini ambao Simba inao basi kuna Wafanyabiashara wanaisupport timu kwa sasa kwa kuwa wana mapenzi nayo ili kulipa hata mishahara.

Kelele hii inadai kuwa tanqu MO DEWJI akabidhi madaraka kwa Salim Abdallah basi ni kama amejiweka pembeni na hatoi mzigo mkubwa kwenye timu hivyo inazidiwa sana kwenye Operational costs ni kuwa timu inazidiwa na mzigo hakuna kwakuwa Dewji amerudi nyuma hatua nyingi.

Nadhani hoja zote mbili zina mashiko, tuanzie hapa kuusaka ukweli! Huu sio muda wa kulaumiana wala kutupiana mipira bali ila mmoja apewe heshima yake kwa kile anachostahili kwenye hii timu, kwa pamoja tufanyie uchunguzi hoja hizi mbili bila kumwonea yoyote.

Mmoja kati ya hawa Wapiga kelele wawili anadanganya je ni nani? Tuwe makini sana nyakati hizi, tusikurupuke! Binafsi nimeanza na hoja YA KWANZA.

Farhan Kihamu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live