Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nchimbi apiga mbili, Yanga yaichapa Alliance kibabe

97558 Yanga+pic Nchimbi apiga mbili, Yanga yaichapa Alliance kibabe

Mon, 2 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Yanga, Ditram Nchimbi ameingia akitokea benchi na kufunga mabao mawili wakati Yanga ikichapa Alliance 2-0 kwenye Uwanja Taifa, Dar es Salaam.

Ushindi huo unaifanya Yanga kuwa katika mazingira mazuri baada ya kutoka sare nne mfululizo kabla ya kuwavaa watani zao wa jadi Simba hapo Machi 8.

Nchimbi aliingia mwanzoni mwa kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Tariq Seif alionyesha ubora wake baada ya kufunga bao la kuongoza katika dakika ya 48, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Mghana Bernard Morrison.

Nchimbi alifunga bao la pili katika dakika ya 79, akitumia vizuri uzembe wa beki wa Alliance FC kushindwa kuokoa mpira wa juu ambao ulitoa mwanya kwa mshambuliaji huyo kuwahi mpira huo na kumchambua kipa Andrew Ntala.

Hilo litakuwa bao la sita la Nchimbi, manne alifunga akiwa na Polisi Tanzania, (hat trick) dhidi ya Yanga na aliwafunga Mwadui FC kabla ya leo kufunga mawili dhidi ya Alliance.

Bao la Nchimbi ni kama limewaamsha Yanga kuanza kutengeneza nafasi zilizokuwa zinawapa presha mabeki wa Alliance, muda mwingi kuzuia mashuti ya hatari.

Pia Soma

Advertisement
Pamoja na Yanga kuonekana hatari zaidi katika safu ya ulinzi ya Alliance, haikuwazuia wapinzani wao kuendelea kushambulia.

Kama si uimara wa beki ya Alliance kuyawahi mashambulizi ya Yanga ingeweza kuruhusu mabao mengi kipindi cha pili.

Alliance ilifanya shambulio dakika ya 71, Deus Cosmas alifanikiwa kumdanganya kipa wa Yanga,Metacha Mnata kama anapiga wakati antoka kuokoa ndipo akapiga lakini bado mlinda mlango wa Jangwani akauokoa.

Dakika ya 75 Nchimbi alifanikiwa kufunga bao la pili la Yanga baada ya kupiga shuti Kali nje ya 18 akiwaacha mabeki wa Alliance nyuma.

Kipa wa Alliance, Ntala alipoona mabeki wake wamepotean akawa akatoka kuuwahi mpira lakini kwa bahati mbaya akapishana nao njiani.

Dakika ya 83 wakati Morrison akitembea juu ya mpira kocha wa timu hiyo alionekana kukasirishwa na tukio hilo akitaka washambulie zaidi.

Wachezaji wa Yanga walionekana kufurahia zaidi ushindi wa mabao mawili ambapo dakika ya 90 Mohamed Jafary aliulia mpira.

KABAMBA KUANZA, METACHA MAPUMZIKO

Awali, kocha wa Yanga, Luc Eymael aliyetumia mfumo wa 4-3-3 alimwanzisha Erick Kabamba kwa mara ya kwanza kwenye timu hiyo akacheza winga ya kushoto kulia akacheza Morrison na kati Tariq.

Pia, Feisal Salum ambaye alipumzishwa kwa kipindi kirefu kutokana na majeruhi kucheza kiungo mkabaji akisaidiana na Haruna Niyonzima aliyekuwa anazunguka uwanja mzima pamoja na Deus Kaseke aliyecheza upande wa kulia huku mabeki wa kati walikuwa Lamine Moro na Juma Said 'Makapu' kulia Juma Abdul na kushoto Jafary Mohammed.

Kipa wa Yanga, Metacha Mnata alitumia dakika 40 za kipindi cha kwanza kupumzika kwa sababu goli lake halikushambuliwa hadi dakika 43, Sameer Vincent alipopiga shuti likatoka nje umbali wa mita moja kutoka kwenye mwamba. Pia, alicheza shuti kali la Martin Kigi dakika ya 75 ambalo kama asingekuwa makini lingekuwa bao.

MORRISON APANDA JUU YA MPIRA MAPEMA

Yanga walianza kwa kasi na kuonyesha wanajiamini, Morrison alianza mapema kuupanda na kuuchezea mpira alipokuwa anamtoka adui katikati ya uwanja dakika ya nne, lakini walijikuta wanamaliza dakika 45, bila bao.

Alirudi tena kufanya 'udambwidambwi' dakika za mwishoni na hii alishirikiana na Niyonzima na Jafary Mohammed ambaye alitembeza mpira kwa tumbo.

Kipa wa Alliance FC, Andrew Ntala alionyesha kiwango cha juu kutokana na kucheza mipira mingi ya hatari kama dakika ya 15 uliopigwa na Tariq Seif na ile zile za nyongeza baada ya 45 kumalizika kabla ya Nchimbi kuokoa jahazi hilo dakika ya 48.

 

VIKOSI

YANGA : 1. Metacha Mnata,  2.Juma Abdul, 3.Jafar Mohammed, 4.Lamine Moro,  5. Said Juma,  6. Feisal Salum,  7. Deus Kaseke, 8. Haruna Niyonzima, 9.Tari Seif/ Ditram Nchimbi ,  10. Erick Kabamba/ Mohammed Issa, 11. Bernard Morrison.

ALLIANCE FC

  1. Andrew Ntala, 2. God love,  3. Makenzi Ramadhani, 4. Joseph James, 5. Geofret Kilele,  6. Shabaan William,  7.Martin Kigi,  8.Juma Nyangi, 9. David Richard, 10.Sameer Vincent, 11. Deus Cosmas.

Chanzo: mwananchi.co.tz