Sun, 27 Mar 2022
Chanzo: eatv.tv
Mlinda mlango wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Costa Rica, Keylor Navas amewachukua wakimbizi 30 wa Ukraine na kuishi nao ndani ya nyumbani yake jijini Paris, Ufaransa.
Navas na mkewe wamenunua vitanda 30 na kuweka katika chumba cha sinema ndani ya nyumba yao kwa ajili ya wakimbizi hao kupata hifadhi, na mkewe amejitolea kuwaandalia chakula kila siku.
Pia Andrea mke wa Navas ametumia ukurasa wake wa instagram kuwaomba watu watoe msaada kwa raia wa Ukraine ambao wameathiriwa na vita dhidi ya Urusi katika ardhi yao ya nyumbani.
Chanzo: eatv.tv