Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nathan Jones ateuliwa kocha mpya Southampton

Skysports Nathan Jones Southampton 5960648 Southampton imemtangaza Nathan Jones

Fri, 11 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Southampton imemtangaza Nathan Jones kuwa kocha wao mkuu akirithi nafasi ya aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Ralph Hasenhuttl huku kocha huyo akisema kuwa ilikuwa ndoto yake kuwa meneja wa timu ya Ligi Kuu England.

Jones ni raia wa Wales, ambaye ana miaka 49, na amepewa mkataba wa kuhdumu ndani ya klabu hiyo hadi 2026.

Southampton wanasema kuwa kazi yake ya kwanza itakuwa kuwaelekeza Watakatifu hao wanaopitia wakati mgumu baada ya kuwa katika nafasi mbaya kwenye msimamo na anatarajiwa abadilishe mwenendo wa timu hiyo.

Jones alisema: “Ninajivunia sana kupewa nafasi hii. Ninajua mengi kuhusu klabu tangu zamani za The Dell, hadi kuja hapa St Mary’s, na ni klabu nzuri ya kandanda, familia yangu wengi ni mashabiki wa Southampton, na ninajisikia fahari sana kupewa nafasi hiyo”

Jones alitumia miaka mitano na nusu katika vipindi viwili kwenye dimba la Luton akiiongoza klabu ya Bedfordshire hadi nusu fainali ya mchujo ya Ubingwa msimu uliopita. Kocha huyo anachukua mikoba ya St Mary’s huku Saints wakiwa nafasi ya 18 kwenye Ligi ya Primia kufuatia msururu wa vipigo sita kutoka kwenye mechi 6.

Mechi inayofuata ya Southampton itakuwa ni dhidi ya Liverpool siku ya Jumamosi na itakuwa ni mechi ya kwanza ya Jones kabla ya mapumziko ya Kombe la Dunia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live