Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Napsa yaiweka pabaya Gor Mahia

F63735537f319904f94fa48e4917a96c Napsa yaiweka pabaya Gor Mahia

Tue, 16 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

GOR Mahia imejiweka njia panda katika mbio zake za kifuzu kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya timu ya Zambia ya Napsa Stars katika mchezo wa kwanza uliofanyika juzi kwenye Uwanja wa Taifa wa Nyayo.

Kiungo Daniel Adoko alifunga bao hilo pekee katika dakika ya 85, na sasa wanasubiri mchezo wa marudiano utakaofanyika Februari 21 kwenye Uwanja wa Mashujaa Lusaka, Zambia huku wenyeji wakiwa na faida ya bao la ugenini.

Adoko mwenye umri wa miaka 21 alitumia vizuri nafasi yake baada ya kupata mpira uliokuwa ukizagaa katika eneo la hatari baada ya beki Geoffrey Ochieng kufanya kosa, baada ya pasi yake kutomfikia mlengwa.

Kocha Mreno Carlos Manuel Vaz Pinto ambaye anaifundisha Gor Mahia kwa mara ya kwanza katika mashindano ya kimataifa tangu aichukue timu hiyo mwezi ulopita kwa ushindi, sasa ana kibarua kizito kucheza hatua ya makundi.

Ushindi huo ni kisasi kizuri kwa kocha wa Misri mwenye umri wa miaka 47 Mohammed Fathi, ambaye alilalamikia mapokezi mabovu wakati walipowasili nchi humo Jumatano, siku nne kabla ya mchezo huo.

Mchezo huo ulihudhuriwa na mashaiki kibao licha ya Shirikisho la Soka la Kenya na serikali awali kusema kuwa utachezwa bila ya mashabiki.

Beki wazamani wa Gor Mahia David Owino 'Calaber', ambaye kwa sasa anaichezea Napsa, alisema ushindi huo umeipa motisha timu yake wakati wakielekea mechi ya marudiano.

Pia alikubali kuwa Gor Mahia wana kikosi dhaifu kwa sasa ukilinganisha na kile kwa mwaka 2015, ambacho alikuwemo na yeye na kushinda taji la Ligi Kuu bila ya kufungwa hata mchezo mmoja.

"Ushindi ni muhimu kwa Napsa na tunatarajia kuendelea kushinda katika mchezo wa marudiano Zambia. Ingawa Gor Mahia ni nyumbani. Nafikiri kikosi cha sasa sio imara sana, “alisema Owino alipozunguza na waandishi wa habari baada ya mchezo huo.

Hatahivyo, mshambuliaji Gor Mahia Nicholas Kipkirui, alisema bado hawajapoteza mchezo huo, kwani watapambana hadi dakika ya mwisho ili kupata nafasi ya kutinga makundi.

"Kutakuwa na mpambano mkali Zambia kwani hakuna mchezaji atakayekuwa tayari kukosa nafasi ya kucheza hatua ya makundi. Ni kipigo kichungu nyumbani, lakini bado hatujapoteza kwani katika soka lolote linaweza kutokea, “alisema Kipkirui.

Chanzo: habarileo.co.tz