Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Napoli yaweka mzigo kwa Lukaku ikimuuza Osimhen

Romelu Lukaku Roma Lukaku

Sun, 9 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Napoli inadaiwa kutuma ofa kwenda Chelsea kwa ajili ya kumsajili Romelu Lukaku dirisha hili la usajili la majira ya kiangazi inayokadiriwa kuwa ni Euro 15 milioni na kuna ongezeko la Pauni 3 milioni kama bonasi ikiwa staa huyo atafanya vizuri.

Mabosi wa Napoli wanapambana kutaka kumsajili Lukaku kwa ajili ya kuziba pengo la Victor Osimhen ambaye ana asilimia kubwa ya kuondoka katika dirisha hili.

Lukaku ambaye mkataba wake na Chelsea unamalizika mwaka 2026, msimu uliomalizika amecheza mechi 47 za michuano yote na kufunga mabao 21, pia ametoa asisti nne.

Mabosi wa Napoli ambao waligoma kumuuza Osimhen katika dirisha lililopita na kumwongeza mkataba, wanataka kutumia pesa watakazopata kwenye mauzo yake ndio watumie kumnunua Lukaku.

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali kutoka Italia, Napoli ipo tayari kumuuza Osimhen kwa dau la Euro 100 milioni au zaidi.

Chelsea inataka kuachana na Lukaku kutokana na mshahara mkubwa anaochukua hivyo wanaweza kukubali ofa hiyo.

Aston Villa huenda ikalazimika kumuuza kiungo wao Douglas Luiz kwenda Juventus dirisha hili ili kuepuka adhabu ya kulimwa pointi kwa kukiuka sheria za matumizi ya pesa kutokana na hali ya mapato na matumizi yao kwa sasa. Luiz ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2026, msimu uliomalizika amecheza mechi 53 za michuano yote, amefunga mabao 10 na kutoa asisti 10.

Bayern Munich imeanzisha tena mazungumzo na Fulham kwa ajili ya kumsajili kiungo wa timu hiyo na Ureno, Joao Palhinha dirisha hili. Taarifa kutoka Skysports zinaeleza Bayern inahitaji kulipa kiasi kisichopungua Euro 45 milioni kwa ajili ya kukamilisha mchakato wa kumnunua. Kiungo huyu wa kimataifa wa Ureno, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.

ARSENAL, PSG na Manchester City bado zimeendelea kuishawishi Newcastle United ili ikubali kuwauzia Bruno Guimaraes dirisha hili licha ya kiungo huyo kuweka wazi hana mpango wa kuondoka kwa sasa. Mkataba wa staa huyu wa kimataifa wa Brazil unamalizika mwaka 2028. Msimu uliomalizika alicheza mechi 50 za michuano yote. Arsenal na PSG zinaonekana kuwekeza nguvu zaidi ili kumsajili.

BEKI wa kushoto wa Arsenal na Scotland, Kieran Tierney, 27, amepanga kurudi Celtic dirisha hili ikiwa timu hiyo itawasilisha ofa ya kutaka kumsajili. Taarifa zinadai Arsenal inataka kumuuza Tierney dirisha hili na tayari baadhi ya timu zimeanza kutuma ofa ka ajili ya kumsajili. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2026. Msimu uliomalizika alicheza mechi 27 za michuano yote.

MANCHESTER City inaendelea kumfuatilia kiungo wa Crystal Palace Adam Wharton, 20, lakini haina mpango wa kumsajili dirisha hili na badala yake inaweza kusubiri kwa msimu mmoja zaidi. Adam ni mmoja kati ya wachezaji vijana wanaofanya vizuri katika timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 21 na 22. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.

WOLVES inajaribu kutaka kumsajili winga wa Braga Rodrigo Gomes, 20, dirisha hili lakini wanakumbana na upinzani mkali kutoka kwa Atletico Madrid inayohitaji huduma yake pia. Gomes kwa sasa ni mmoja kati ya mastaa tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Braga na msimu uliomalizika alicheza mechi 36 za michuano yote na kufunga mabao tisa.

LEICESTER City inapambana kwa nguvu zote kuhakikisha kiungo wao Wilfred Ndidi anaendelea kubaki King Power baada ya Mnigeria huyo kuwindwa na miamba ya soka ya Hispania, Barcelona. Ndidi mkataba wake unafika tamati mwisho wa mwezi huu na Foxes wamekuwa wakisisitiza watafanya kila wanaloweza kumsainisha mkataba mpya kiungo huyo ili abaki kwenye kikosi chao.

Chanzo: Mwanaspoti