Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Napoli yakana kuuzwa kwa klabu hiyo

Skysports Aurelio De Laurentiis 5091930 Rais wa Napoli, Aurelio De Laurentiis

Thu, 21 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Napoli inayoshiriki ligi kuu ya Italia Serie A imepinga taarifa zilizosambazwa na vyombo vya habari nchini humo kuwa klabu hiyo imeuzwa.

Vituo kadhaa vya runinga nchini humo vikiongozwa na kituo cha serikali Rai, vilieleza kuwa klabu hiyo imefikiana makubaliano ya kuuzwa kwa klabu hiyo kwa kiasi kinachokadiriwa kufikia €650 million.

“Kwenye hali yoyote ya kawaida, taarifa kama hii tusingehitaji kukataa lakini taarifa ya Rai kama chombo cha serikali wametulazimisha kusema hili. De Laurentiis hana nia ya kuiuza Napoli na hakuna mazungumzo yoyote.

“Awali, hapo nyuma, alikataa ofa inayokaribia $1 billion. Kuibuka kwa tetesi ni kwa sababu raisi De Laurentiis kuwa angependa kuishi Marekani.

“De Laurentiis amekuwa akiishi jijini Los Angeles na Italia na hivi karibuni amerejea kwa miezi kadhaa kutoka kwenye makazi yake ya muda mrefu.

“Haitaji kuiuza Napoli kwa ajili ya kuhamia Marekani pindi kazi zake zikimuhitaji.”

De Laurentiis, aliinunua klabu ya Napoli mwaka 2004 kipindi ambacho klabu hiyo ilikuwa miongoni mwa klabu tabu ambazo zilikuwa zinakwenda kufirisika.

De Laurentiis mara kwa mara amekuwa akipongezwa kwa utendaji na usimamizi mzuri wa klabu hiyo na kuwa klabu pekee kwenye serie A kutengezeneza faida mara kwa mara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live