Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Napoli wachezea kichapo nyumbani

Fiorentina 169.jpeg Napoli wachezea kichapo nyumbani

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi wa Serie A, Napoli ambayo ipo chini ya kocha mkuu Rudi Garcia wamechezea kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Fiorentina.

Mabingwa hao wamekuwa wakisuasua msimu huu kwenye mechi zao ambazo wamecheza huku wakipoteza mechi mbili za ligi hadi sasa na wanashikilia nafasi ya 5 wakiwa na pointi zao 14.

Lakini pia wamepoteza mchezo wa ligi ya mabingwa wakiwa hapo hapo nyumbani, na hii ni kuonyesha kuwa wana dalili ndogo sana za kutwaa mataji makubwa msimu huu barani Ulaya.

Chini ya kocha mpya Garcia Napoli wamekuwa hawapigiwi chapuo la kuchukua Scudeto msimu huu kwani mpaka sasa wameachwa pointi 7 na kinara wa ligi ambaye ni AC Milan mwenye pointi 21.

Baada ya mapumziko ya Kimataifa, Naples watakipiga dhidi ya Hellas Verona ugenini na baada ya hapo tarehe 24 watarejea kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa mabao watakuwa ugenini dhidi ya Union Berlin ya Ujerumani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live