Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Napol yaitaka saini ya Lukaku kwa mkopo

Napol Yaitaka Saini Ya Lukaku Kwa Mkopo.png Napol yaitaka saini ya Lukaku kwa mkopo

Tue, 20 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tetesi za usajili zinasema klabu ya Napoli imewasilisha ofa kumsajili Romelu Lukaku kwa mkopo huku kukiwa na chaguo la kumnunua kwa pauni milioni 25.5.

Lukaku, aliyejiunga na Chelsea mwaka 2021 kwa ada ya pauni milioni 98 aliachwa katika kikosi cha kocha Enzo Maresca kilichopokea kichapo cha mabao 2-0 toka kwa Manchester City Agosti 17 katika mchezo wa ufunguzi Ligi Kuu England na hajacheza The Blues kwa zaidi ya miaka miwili.

Ametumikia misimu miwili iliyopita kwa mkopo katika klabu za Inter Milan na Roma, mtawalia, na sasa anaweza kurudi tena Italia kuchezea klabu ya tatu tofauti.

Chelsea inasisitiza kwamba inataka kumuuza Lukaku kwa ada inayokaribia kipengele cha kumwachia cha pauni milioni 36 huku fowadi huyo akiwa bado ana miaka miwili imebaki katika mkataba wake Stamford Bridge.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live