Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nape: Msitumie mitandao ya kijamii kutukana matapeli

Nape Nnauye Taswa Nape: Msitumie mitandao ya kijamii kutukana matapeli

Tue, 16 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amekagua minara iliyojengwa na kampuni mbili za mawasiliano Nchini ambapo Serikali imechangia ruzuku ya zaidi ya Tsh. milioni 278.4.

Minara hiyo imejengwa katika eneo la Kumbanga na Bunyambo ambayo inatoa huduma kwa Wananchi wa Kijiji cha Kumbanga, kumhasha, sehemu ya kambi ya Wakimbizi ya Nduta, Bunyambo Bavunja, Minyinya na Samvura.

Akiongea na Wananchi wa Vijiji hivyo Waziri Nape amewataka Vijana na Watumiaji wengine wa mitandano ya mawasiliano kuitumia kwa ajili ya kujipatia maendeleo, kujenga umoja na mshikamano.

“Ndugu zangu Serikali inafanya uwekezaji mkubwa kwenye mawasiliano, nawaomba tuitumie kwa mambo mazuri ikiwemo kukuza maendeleo yetu kiuchumi na jamii ili Rais wetu (Samia Suluhu Hassan) aendelee kuona manufaa ya uwekezaji huu ili azidi kutoa maelekezo fedha nyinyi zitumike kuimarisha mitandao ya mawaliliano Nchini”

Nape amewataka Watumiaji wa mitandao kuacha tabia ya kuitumia kwa kutukana Viongozi, kueneza vitu vya hovyo na vya uzushi pamoja na kuacha vitendo vya utapeli kwenye mitandao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live