Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nanyumbu waanzisha kidato cha tano na sita

18beda94c8be14afde32d94e74ea827d Nanyumbu waanzisha kidato cha tano na sita

Sun, 1 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

HATIMAYE Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara imeanzisha kidato cha tano na sita wilayani humu ili kuhakikisha wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne wanaendelea na masomo wilayani humo.

Mkurungezi Mtendaji wa Halmashauri wa Wilaya ya Nanyumbu, Hamisi Dambaya, alisema Shule ya Sekondari ya Mangaka ameanisha kidato cha tano na sita na tayari serikali imetoa Sh million 120 kujenga madarasa na mabweni yatakayotumiwa na wanafunzi wanaojiunga na kidato cha tano na sita shuleni hapo.

"Ni faraja kwetu sisi watu wa Nanyumbu kuanzisha kidato cha tano, kwa sasa tunaendelea na upanuzi wa miundombinu katika Shule ya Sekondari ya Mangaka na sasa tunaendelea na upanuzi wa miundombinu katika shule yetu ya Sekondari Mangaka amabyo ndiyo ina A-level," alisema.

Dambaya alisema Shule ya Sekondari ya Mangaka ina bweni linalochukua wanafunzi 40 na kwamba, fedha ilizopata halmashuri hiyo kutoka serikalini inazitumia kujenga bweni lingine pamoja na madarasa mawili yanayotumiwa na wanfunzi kidato cha tano na sita.

Alisema baada ya halmashauri yake kuomba kuanzishwa kwa kidato cha tano na sita katika wilaya hiyo mwaka huu, wanafunzi 84 wamedahiliwa katika shule hiyo hukuwalimu 12 wakiongezwa katika shule hiyo ili kuongeza nguvu katika ufundishwaji wa wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne na kidato cha tano na sita.

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mangaka, Geofray Kiula, alisema uamuzi wa serikali kuanzisha kidato cha tano na sita katika wilaya hiyo umeleta mwamko kwa wanafunzi pamoja na wazazi,

"Hatua hii imekuwa chachu kwetu kwa sababu tumehamasika kuona kwamba kumbe inawezekana watoto wetu kujifunza na kuendelea kidato cha tano na sita na kuona kwamba mtoto amefaulu kidato cha nne na kuendelea na kidato cha tano na sita hapa hapa shuleni," alisema Kiula.

Chanzo: habarileo.co.tz