Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nani kuvaa kitambaa cha unahodha Arsenal?

Gunners Cap Arsenal imemvua unahodha Aubameyang kwa makosa ya kinidhamu

Wed, 15 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vita ya nani atakuwa nahodha mpya wa Arsenal bado, kutatuliwa kutokana na kocha mkuu wa Arsenal Mikel Arteta kusema kuwa hana haraka ya kumchagua mchezaji atakaye vaa kitambaa cha unahodha kwenye klabu hiyo.

Pierre-Emerick Aubameyang amevuliwa kitambaa cha unahodha wa klabu hiyo kutokana na utovu wa nidhamu aliouwonyesha klabuni hapo

Kwa sasa Arsenal wanatafuta mbadala wa Pierre-Emerick Aubameyang, ambaye ataingoza timu kwenye vipindi muhimu na kuhamasisha wachezaji wenzake, huku kocha mkuu wa Arteta akisema kuwa hana haraka ya kumchagua nahodha wa kudumu kwa sasa.

kuna tetesi kuwa Gabriel, Kieran Tierney, Granit Xhaka, Martin Odegaard, Ben White, Alexandre Lacazette na Aaron Ramsdale wanahusishwa kati yao ndipo jina la nahodha mpya wa washika bunduki wa London ndipo litakapotoka. Nani ataibuka kati yao?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live