Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nani kuibuka mbabe Fainali ya EURO 2024 leo?

Nba Canada  57554788 86a4 41d3 9c67 8138cc84b6fc.png Nani kuibuka mbabe Fainali ya EURO 2024 leo?

Sun, 14 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Leo ndio kilele cha michuano ya Euro 2024 ambapo Hispania na England zitakutana kwenye Uwanja wa Olympiastadion jijini Berlin, Ujerumani, kuanzia saa 4:00 usiku ikitarajiwa kuwa ni fainali ya maokoto kwa timu itakayoshinda.

Kwa mujibu wa The Sun, wachezaji wa Hispania kila mmoja atapata Pauni 300,000 ikiwa watashinda mechi hiyo na kuchukua ubingwa, huku England ikitarajiwa kupata zaidi.

Mastaa wa Hispania wameahidiwa kiasi hicho cha pesa baada ya mazungumzo na mabosi wa Chama cha Soka cha Hispania (RFEF) kilichofanyika baada ya kutinga fainali.

Kikao hicho ambacho kiliongozwa na mastaa tegemeo kama Rodri na Alvaro Morata, kilifikia muafaka kwamba kila mchezaji katika kikosi ikiwa ni pamoja na benchi la ufundi wote watapata bonasi ya Pauni 306,646 ambao ndio utakuwa mkwanja mkubwa zaidi kulipwa kama bonasi katika historia ya timu ya taifa ya Hispania.

Kwa mujibu wa ripoti, mkwanja huo wa bonasi utatoka katika zawadi ambayo Hispania itapata kwa kushinda michuano hiyo, ambapo jumla ya pesa zote zinatarajiwa kuwa ni Euro 28.5 milioni na wachezaji waliambiwa kwamba watapata asilimia 40 ya pesa hiyo ambayo itakuwa Euro 11.3 milioni. Kiasi hicho kitagawanywa kwa watu 31.

Kwa upande wa England ikiwa watashinda mechi na kuchukua ubingwa, wachezaji wanatarajiwa kukunja pesa nyingi zaidi.

Gazeti la The Sun linaeleza wachezaji watapewa Pauni 9.6 milioni wagawane ikiwa watabeba kombe na kwa makadirio kila mchezaji anaweza kupata Pauni 369,000.

Mbali ya wachezaji kuvuna mkwanja wa maana, kocha Gareth Southgate ana bonasi ya pekee ikielezwa kwamba atakunja mzigo wa Pauni 4 milioni.

Kiasi hicho cha fedha kitamuwa ni mara 10 zaidi ya kile ambacho kocha wa Hispania, De La Fuente atapata ambacho ni sawa na wachezaji wake kama ilivyoelezwa hapo juu.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (Uefa), limeandaa Euro 331 milioni ambazo litazigawa kwa timu shiriki kulingana na nafasi zinazomaliza kuanzia makundi hadi bingwa.

Kwanza, kwa kufuzu tu timu zote 24 kila moja imepata Euro 9.25 milioni na katika makundi kila mechi ambayo timu ilishinda ilipata Euro 1 milioni na sare Euro 500,000.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live