Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika inafikia tamati leo Mei 25, 2025 kwa mchezo mmoja wa fainali ya mkondo wa pili kati ya bingwa mtetezi, Al Ahly dhidi ya vigogo wa Tunisia, Esperance Tunis katika dimba la Al Salam, Cairo.
Al Ahly wanatazamia kutwaa ubingwa wa Afrika kwa mara ya 12 huku wakihitaji kutetea ubingwa huo kwa kutwaa kwa mara ya pili mfululizo.
ES Tusis wanaangazia kutwaa kombe hilo kwa mara ya 5 kihistoria na kwa mara ya kwanza tangu 2019 walipowafunga Wydad Casablanca kwenye fainali.
Vigogo hao wa Tunisia pia wana malengo ya kuwafunga Al Ahly kwa mara ya pili mfululizo kwenye fainali ya michuano hiyo baada ya kuwachapa kwa matokeo ya jumla ya 4-3 kwenye fainali mnamo 2018.
Al Ahly ina faida ya kutumia uwanja wake wa nyumbani baada ya mchezo wa mkondo wa kwanza kumalizika kwa sare tasa huko Tunisia.
20:00 | Al Ahly vs Esperance
Uwanja: Al Salam, Cairo