Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nani kubeba CHAN leo, Algeria au Senegal?

Algeria Kati Ya Senegal .jpeg Nani kubeba CHAN leo, Algeria au Senegal?

Sat, 4 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani(CHAN) inapigwa leo huko Algeria kati ya Senegal na wenyeji Algeria.

Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja mpya wa Nelson Mandela uliofunguliwa Januari 7, 2023 uliopo kitongoji wa Baraki katika mji mkuu wa nchi hiyo, Algiers.

Algeria imetinga fainali baada ya kuichakaza Niger kwa mabao 5-0 wakati Senegal imeitoa Madagascar kwa bao 1-0.

Ikumbukwe Senegal ndio mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON) baada ya kuifunga Misri kwa mikwaju ya penalti 4-2 katika fainali kwenye uwanja wa Olembe, Yaounde Cameroon Februari 6, 2022.

Mshindi wa tatu wa CHAN ni Madagascar baada ya kuifunga Niger kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa kutafuta nafasi hiyo uliopigwa Februari 3.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live