Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nani atapiga bao la kwanza Qatar?

Nikica Jelavic And Ivan Perisic Of Croatia Celebrate As Marcleo alijifunga bao la kwanza michuano ya Kombe la Dunia 2014

Sun, 30 Oct 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Fainali za Kombe la Dunia 2022, wenyewe watakata utepe kwa kuwakabili Ecuador katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi A utakaopigwa Novemba 20 uwanjani Al Bayt.

Mashabiki wa soka duniani wanasubiri kuona ni mchezaji gani atakuwa wa kwanza kufungua akaunti ya mabao yatakayofungwa kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia 2022. Atakuwa mchezaji wa Qatar mwenyeji wa fainali hizo au atatokea kwenye kikosi cha Ecuador?

Hii hapa orodha ya wanasoka waliofunga mabao ya kwanza kwenye fainali za Kombe la Dunia kuanzia mwaka 1930.

Lucien Laurent, Ufaransa (1930)

Hili ndilo bao la kwanza kufungwa kwenye historia ya fainali za Kombe la Dunia. Kwenye mechi hii ya ufunguzi ya Kombe la Dunia 1930, Ufaransa iliifunga Mexico mabao 4-1.

Pal Teleki, Hungary (1934)

Bao hili lilifungwa dakika ya 11 kwenye mechi ya ufunguzi wa fainali za 1934 kule Italia. Hungary iliichapa Misri mabao 4-2.

Pietro Ferraris, Italia (1938)

Fainali za mwaka 1938 zilizofanyika Ufaransa, Italia iliifunga Norway mabao 2-1 huku bao la kwanza likifungwa na Ferraris wa Kikosi cha Azzurri.

Ademir Menezes, Brazil (1950)

Wenyeji walifungua vyema fainali hizi kwa kuichapa Mexico 4-0 kwenye mechi ya ufunguzi. Bao la kwanza lilifungwa na Menezes dakika ya 30.

Oswaldo da Silva Baltazar, Brazil (1954)

Brazil ilipata nafasi ya kufungua tena na Mexico na ilizidi kuonyesha ubora wake ikishinda 5-0, huku bao la kwanza likifungwa na Baltazar dakika ya 23 ya mchezo.

Oreste Corbatta, Argentina (1958)

Corbata alihitaji dakika tatu tu kufunga bao la kwanza la fainali za Kombe la Dunia 1958. Staa huyo wa Argentina alifunga bao hilo dhidi ya Ujerumani Magharibi.

Francisco Zuluaga, Colombia (1962)

Fainali za mwaka 1962 ulikatwa na Zuluaga wa Colombia kwa bao lake la dakika ya 19 kwa mkwaju wa penalti.

Enrique Borja, Mexico (1966)

Baada ya mechi ya ufunguzi kuisha kwa sare ya 0-0, Borja alikata utepe kwa kufunga bao la kwanza la fainali hizi dhidi ya Mexico na Ufaransa.

Wilfried Van Moer, Ubelgiji (1970)

Ndiye aliyefumania nyavu kwa mara ya kwanza dakika ya 12, fainali za Kombe la Dunia 1970 huko Mexico.

Paul Breitner, Ujerumani Magharibi (1974)

Breitner alifunga bao hili dakika ya 18 na kuiwezesha Ujerumani kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chile.

Bernard Lacombe, Ufaransa (1978)

Moja kati ya mabao ya mapema kwenye mechi za ufunguzi. Lacombe alifunga bao hili dakika ya kwanza kwenye mchezo dhidi ya wenyeji Argentina.

Bruno Conti, Italia (1982)

Fainali za mwaka 1982 bao la kwanza lilifungwa na Conti wa Italia dakika ya 18.

Alessandro Altobelli, Italia (1986)

Alikata utepe wa fainali za mwaka 1986 zilizofanyika Mexico dakika ya 44.

Salvatore Schillaci, Italia (1990)

Italia iliendelea kukata utepe kwenye fainali za tatu mfululizo baada ya Schillaci kufunga bao la kwanza la fainali hizo.

Georges Bregy, Uswisi (1994)

Fainali hizi zilizofanyika Marekani zilifunguliwa rasmi kwa bao la Bregy wa Uswisi dakika ya 39.

Cesar Sampaio, Brazil (1998)

Sampaio ndiyo alizizindua nyavu za fainali za mwaka 1998 kule Ufaransa baada ya kufunga bao la kwanza dakika ya tano.

Papa Bouba Diop, Senegal (2002)

Hapa ilikuwa zamu ya Waafrika baada ya staa wa Senegal, Papa Bouba Diop kukata utepe wa fainali hizo dakika ya 30.

Philipp Lahm, Ujerumani (2006)

Fainali hizi zilifanyika Ujerumani na Wajerumani wenyewe ndiyo walikata utepe wa fainali hizi kwa bao la Philipp Lahm katika dakika ya sita ya mchezo.

Siphiwe Tshabalala, Afrika Kusini (2010)

Afrika Kusini wakiwa wenyeji wa fainali za Kombe la Dunia 2010, mechi yao ya kwanza walikipiga na Mexico, ambapo staa wa nyumbani, Siphiwe Tshabalala aliingia kwenye rekodi ya kufunga bao la kwanza kwa shuti kali dakika ya 55.

Marcelo, Brazil (2014)

Mcheza kwao hutuzwa watu husema na hapo, staa mwingine wa nyumbani alikata utepe kwa kufunga bao kwenye fainali za Brazil. Marcelo ndiye aliyefunga bao la kwanza dakika ya 11 tu ya mchezo.

Yuri Gazinsky, Russia (2018)

Kwa mara ya tatu mfululizo kwenye fainali za Kombe la Dunia, bao la kwanza linafungwa na mchezaji wa timu mwenyeji, ambapo Russia 2018, mchezo wao wa kwanza iliichapa Saudi Arabia 5-0, huku bao la kwanza likifungwa na Yuri Gazinsky.

Chanzo: Mwanaspoti