Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nani alistahili kuwa Ma of the Match?

Bacca Mustapha 0005 Nani alistahili kuwa Ma of the Match?

Mon, 3 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kumeibuka mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu nani alipaswa kuwa mchezaji bora wa mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB jana usiku ambapo Yanga aliibuka na ushindi kwa changamoto ya mikwaju ya penati na kufanikiwa kubeba taji hilo kwa mara ya 8 sasa tangu lianzishwe.

Wengi wanasema beki wa Yanga, Abdul Hamad Ibrahim Yanga hakupaswa kupewa tuzo hiyo na badala yake angepatiwa kipa wa Azam, Mustapha kutokana na kazi kubwa aliyoifanya kwenye mechi hiyo ikiwemo kufanya saves nne na kuondoa hatari ambazo zingezaa mabao na hata kuokoa mikwaju miwili ya penati.

Hans Raphael, Mchambuzi wa masuala ya soka anasema; "Mimi ni shabiki mkubwa wa Ibrahim Bacca na kwa kweli leo amepiga Kazi haswa, amechaguliwa kuwa MAN OF THE MATCH wa fainali ya CRDB Federation cup 23|24, amekunja Tsh 1 Million.

"Lakini binafsi naona tuzo hii alistahili Golikipa wa Azam FC, Mustafa. Huyu jamaa ndiye aliyesababisha mechi iende mpaka dakika 120', kama si ubora wake golini Azam FC wangepigwa (0-3) ndani ya dakika (90') tu. Kafanya saves (4) hatari Hans Raphael.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live