Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nani alisema Aziz Ki hafungi?

Aziz  Ki Yanga Ml Aziz Ki

Wed, 14 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ushindi wa mabao 3-0 ambao Yanga imeupata dhidi ya Mtibwa Sugar umeifanya timu hiyo kuishusha Azam kwenye kilele cha msimamo wa Ligi Kuu NBC uliochezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Awali Azam ilikuwa ikiongoza msimamo huo wakiwa na pointi nane baada ya kuifunga Mbeya City bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Mabao ya Shaaban Djuma, Fiston Mayele na Azizi Ki yamewafanya mashabiki wa Yanga kuondoka katika uwanja wa Benjamin Mkapa vifua mbele kufuatia timu yao kuvuna pointi tatu.

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki amefanikiwa kufunga bao lake la kwanza kwenye ligi dakika ya 90 katika mchezo huo, huku kinara wa ufungaji wa timu hiyo Mayele akifikisha mabao matatu kwenye ligi nyuma ya Reliant Lusajo wa Namungo mwenye manne.

Bao la ufunguzi katika mchezo huo lilifungwa na beki Djuma Shabaan dakika ya 33 akipiga mpira wa faulo aliochezewa Farid Musa nje kidogo eneo la hatari ambao ulimshinda Kipa wa Mtibwa Farouk Shikalo na kujaa wavuni.

Simba ambayo ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi saba sawa na Namungo huku mchezo wao wa nne ukiwa dhidi ya Tanzania Prisons utachezwa kesho, Jumatano kwenye dimba la Sokoine, Mbeya.

Wakati Simba aikikipiga dhidi ya Prisons, Namungo atakuwa nyumbani kuikaribisha Coastal Union ya Tanga.

Kikosi cha Yanga, Djigui Diarra, Djuma Shaaban, Kibwana Shomary, Dickson Job, Yannick Bangala, Khalid Aucho, Salum Abubakar 'Sureboy', Jesus Moloko, Feisal Salum, Fiston Mayele, Farid Mussa.

Upande wa Mtibwa Sugar, Farouk Shikhalo, David Kameta, Issa Rashid,  Cassian Ponera, Vedastus Mwihambi, Pascal Kitenge, Ismail Mhesa, Balama Mapinduzi, Charles Ilamfia, Adam Adam, Nickson Kibabage.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live