Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nani ajifunze kwa mwenzake, Manula au Diarra?

WhatsApp Image 2021 03 02 At 10.jpeg Aishi Manula

Fri, 31 Dec 2021 Chanzo: Mitandao

Kuna kamjadala kanatembea huko mitandaoni juu ya ubora wa makipa wawili Manula wa Simba na Diarra wa Yanga. Nani bora? Nani anastahili kujifunza kwa mwezake? Haya ndiyo maswali wanayojiuliza watu wengi.

YES ni maswali fikirishi. Wote ni makipa bora Mosi. Pili sidhani kama Aishi ana cha kujifunza kwa Diarra au Diarra ana cha kujifunza kwa Aishi. Wote wana safari ndefu, lakini kuna sehemu Manula yuko Diarra hayuko.

Simba na Taifa Stars zimemtangaza Manula kwa kiasi kikubwa. Kitendo cha Simba kucheza robo fainali mbili ndani ya miaka minne kimemfanya ajitangaze Afrika, sio kwa jina lake. Bali uwezo. Nchi nyingi zinamjua Aishi.

Diarra ni moja ya makipa mahiri walioko katika soka letu kwa sasa. Huu ni ukweli usiopingika, lakini anapaswa kufanya kazi. Atuonyeshe kama ambavyo Aishi ametuonyesha na anatuonyesha katika mechi za ligi na mechi za kimataifa.

Aishi amewahi kwenda Misri na Simba akachukua 5-0. Amewahi kwenda Congo na Simba akachukua tena 5 -0 nyingine. Vipigo hivyo vimemuimarisha kwa kiasi kikubwa. Tunataka kumuona Diarra katika level hizi, sio mtu atuambie moja kwa moja Diarra ni bora kumzidi Aishi.

Katika taifa la Mali ambalo ni kubwa kuliko letu Diarra ni kipa namba mbili. Aishi ni namba moja wa Tanzania.

Hatujui kama Diarra angekuwa Mtanzania au Manula angekuwa M'mali nini kingetokea kati yao kwenye lango.

Manula ana uzoefu mkubwa wa kusimama langoni dhidi ya washambuliaji mahiri wakubwa wa Afrika. Uzoefu wa Diarra anaupata katika benchi. Japo hili sio la kubeza.

Inawezekana Diarra angekuwa Mtanzania huenda ndiyo angekuwa ndiyo Tanzania One. Inawezekana.

Nadhani Watanzania hatupaswi kujipa presha ya kuwafananisha hawa makipa wawili. Diarra anatakiwa kufanya sana kazi ndiyo tuje katika meza ya ubishani.

Aliko sasa Manula haitaji tena maswali. Amefanya kazi kubwa na kila mmoja wetu ameiona. Kina Metacha, Haroun Mandanda, Mussa Mbise na wengineo ndiyo wanapaswa kujifunza kwa Diarra, sio Manula.

Kama Manula anataka kujifunza kitu awatazame kina Mohammed El Shanawy, Dennis Onyango, Sharrif Ekramy, Ithumeleng Nkune, lakini sio Diarra.

Chanzo: Mitandao