Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namungo yawachunia makocha 10 wapya

Namungoi Waichapa Azam FC Namungo FC.

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Namungo umesema licha ya kupokea maombi mengi ya makocha kutoka ndani na nje ya Tanzania kutaka kuinoa timu hiyo, lakini hautakurupuka haraka isipokuwa kwa sasa majukumu ya benchi la ufundi yapo kwa Denis Kitambi.

Namungo inayoshiriki ligi hiyo kwa msimu wa nne sasa, hauna kocha mkuu baada ya aliyekuwapo, Cedrick Kaze kung’atuka mwenyewe kufuatia matokeo yasiyoridhisha.

Katibu mkuu wa timu hiyo, Ally Suleiman alisema zaidi ya makocha 10 kutoka mataifa mbalimbali Afrika wamewasilisha maombi lakini bado hawajaamua kufanya uamuzi wa kumpa yeyote kazi.

Alisema kwa sasa wamemua kumpa majukumu Kitambi ambaye alikuwapo tangu msimu uliopita akisaidiana na Shadrack Nsajigwa kuhakikisha anawavusha katika michuano hiyo.

“Tuna maombi ya makocha kutoka Rwanda, Cameroon, Comoro, Tunisia, Uganda, Nigeria Congo pamoja na wengine kutoka hapa Tanzania, lakini hatujafikiria kumkubalia yeyote,”

“Tunasubiri kuona Kitambi na Nsajigwa watatuvushaje katika mechi zinazofuata, hatujawa na matokeo mazuri lakini tunaamini tutasimama vizuri,” alisema Suleiman.

Kigogo huyo aliongeza kuwa uongozi unaendelea kutoa sapoti na kuwa karibu na timu kuhakikisha wachezaji wanakuwa na morali ili kupambania pointi tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: