Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namungo yatoa kauli ya kibabe kwa Vigogo

Namungo Ubingwa Namungo yatoa kauli ya kibabe kwa Vigogo

Thu, 3 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Yanga na Simba zikipapatuana katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara, Namungo imeongeza presha ikisisitiza inalihitaji taji hilo msimu huu.

Hadi sasa timu hiyo ya mkoani Lindi ipo nafasi ya tatu kwa pointi 15 baada ya kucheza mechi tisa ikiachwa alama mbili na Wekundu wa Msimbazi, huku Yanga ikiongoza msimamo kwa pointi 20 baada ya kushuka uwanjani mara nane.

Namungo ambayo inashiriki ligi hiyo kwa msimu wa nne sasa, haijawahi kutwaa ubingwa wowote tofauti na kumaliza ndani ya nafasi nne za juu na kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2020/21 na kufuzu hatua ya makundi.

Akizungumza nyota wa timu hiyo, Shiza Kichuya alisema msimu huu nao wanautaka ubingwa kutokana na matokeo waliyoanza nayo, pia ubora na uwezo wa wachezaji wote kwa jumla.

“Hata sisi Namungo malengo yetu ni ubingwa msimu huu, ndio maana tunapambana kila mechi kupata pointi, tumejipanga na tumeazimia kufikia ndoto, tunachoomba ni sapoti kwa mashabiki,” alisema Kichuya.

Winga huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar na Simba, aliongeza hata ishu ya ufungaji bora kwake inawezekana kwani mabao matatu aliyoachwa na vinara, Reliant Lusajo (Namungo) na Moses Phiri wa Simba anaweza kuyafikia na hata kuyapita.

Kocha msaidizi wa Namungo FC, Shadrack Nsajigwa alisema kwa sasa wao wanapambana na mechi zao bila kuangalia wapinzani kisha kusubiri mwisho wa msimu kujua hatma yao.

“Sisi hatuchezi kuwaangalia walio nyuma au mbele yetu, tunachopambania ni kupata ushindi katika kila mchezo,” alisema nyota huyo wa zamani wa Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live