Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namungo yanogewa, yataka wengine wawili

Namungo+pic Namungo yanogewa, yataka wengine wawili

Sat, 8 Aug 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By YOHANA CHALLESIKU chache baada ya kudaiwa kumnyakua Shiza Kichuya kutoka Simba, Namungo FC ni kama wameanza kunogewa na sasa wameanza hesabu za kuwachomoa nyota wawili kutoka Mtibwa Sugar.

Mwenyekiti wa Namungo, Hassan Zidadu amethibitisha wanaisaka saini ya beki, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ pamoja na kiungo fundi wa mpira, Abdulhalim Humoud ‘Gaucho’ ikiwa ni sehemu ya mipango yao ya kuimarisha kikosi chao kitakachoiwakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

“Ripoti ya kocha aliyowasilisha mezani imeeleza maeneo ya kuimarisha na pia imependekeza kwa kuwataja majina ya wachezaji kadhaa wakiwemo hao wawili,” alisema Zidadu na kuongeza;

“Upande wetu hatuna pingamizi na kile anachokitaka kocha, yeye ndiye aliyewachagua na kuona wanafaa na kilichobaki ni kuwasiliana na uongozi wa Mtibwa ili tujue kama wachezaji hao bado wana mkataba ama wapo huru,” alisema Zidadu.

Aliongeza watajitahidi kufuata yale yote aliyoyataka kocha kwa ajili ya msimu ujao na kuyatekeleza ili timu itakapofanya vibaya isionekane uongozi uliingilia majukumu.

“Kwa Humoud amesema uzoefu wake utaisaidia timu katika michuano ya kimataifa, huku Baba Ubaya amependekezwa kutokana na namna anavyojua kufanya kazi vyema kwenye nafasi yake kama beki.”

Chanzo: mwanaspoti.co.tz