Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namungo yambana Mudathir mapema

Mudathir Yahya Simuu Namungo yambana Mudathir mapema

Thu, 7 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kusota kwa dakika 450 bila kupata ushindi hatimaye Namungo juzi usiku ilizinduka kwa kuichapa Kagera Sugar bao 1-0 lililofungwa na Ibrahim Mkoko, huku ikitamba nguvu iliyopata inahamia kwa Yanga ikiisaka rekodi ya kwanza dhidi ya kinara hao wa Ligi Kuu.

Namungo ilikuwa haijaonja ushindi kwenye mechi tano mfululizo za Ligi Kuu kabla ya juzi usiku kuzinduka na kuifanya ipande kutoka nafasi ya 11 hadi ya saba ikifikisha pointi 23 na kesho itakuwa wenyeji wa Yanga ambayo hawajawahi kuifunga tangu waanze kucheza Ligi Kuu msimu wa 2020.

Ushindi huo ulikuwa wa kwanza raundi ya pili kwa timu hiyo baada ya kuwa ugenini michezo mitano iliyocheza bila kuonja pointi tatu na sasa watakuwa uwanjani tena dhidi ya Yanga, huku ikisaka rekodi ya kupata ushindi wa kwanza kwa wababe hao kwani haijawahi kuifunga timu hiyo.

Kabla ya ushindi huo, ilipoteza mechi mbili dhidi ya Tanzania Prisons 1-0 kipigo sawa na Mashujaa, ikitoa sare tatu mbele ya KMC, 2-2, suluhu ya kutofungana na JKT Tanzania na Tabora United 1-1.

Katika misimu mitano ilizokutana na Yanga katika Ligi Kuu, Yanga imeshinda mechi tano sawa na sare, huku vigogo hao wakikumbuka kumuachisha kazi aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Cedrick Kaze kufutia kichapo cha 1-0 raundi ya kwanza na kwa sasa timu hiyo inanolewa na kocha wa zamani wa Yanga na Coastal Union, Mwinyi Zahera.

Nahodha wa Namungo, Jacob Massawe alisema matokeo ya ushindi walioupata imewaweka sawa kisaikolojia na sasa akili na nguvu zinafikiria mchezo ujao dhidi ya Yanga kuvunja uteja.

Alisema watakuwa makini na mambo matatu ikiwa ni kumdhibiti kiungo Mudathir Yahya ambaye amekuwa mwiba kufunga mabao ya dakika za mwisho, kutokubali kuruhusu mabao matano kama timu nyingine.

“Lakini kutoruhusu bao la mapema linaloweza kutotoa mchezoni na kutoendeleza uteja kwa wapinzani hao licha ya kuwaheshimu kwa ubora walionao hivi sasa.”

Chanzo: Mwanaspoti