Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namungo yaliamsha mapemaa

Namungo Killers Namungo yaliamsha mapemaa

Sat, 1 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kikosi cha Namungo kimerejea mazoezini kuiwinda Mbeya City watakaokutana nayo Aprili 9 kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi, huku kocha mkuu wa timu hiyo, Dennis Kitambi akisema ana kazi ya kuiimarisha safu yake ya ulinzi.

Kitambi alisema changamoto waliyonayo kwa sasa ni kwenye safu ya ulinzi kwani imekuwa ikiruhusu mabao katika mechi za karibuni.

Katika mechi nne zilizopita, Namungo imeruhusu mabao saba, ilichapwa na Yanga mabao 2-0, ikafungwa na Kagera bao 1-0, iliifunga Geita Gold mabao 2-1 na ikatandikwa na Prisons mabao 3-2. Kitambi amesema wanahitaji kuifanyia marekebisho safu yao ya ulinzi ili wamalize vizuri michezo yao mitano ya ligi iliyobaki msimu huu.

“Tumerudi mazoezini na kubwa tunaloliangalia ni hilo ili kwa sababu katika mechi tatu zilizopita tumeruhusu mabao mengi.

“Sasa tunataka kuhakikisha mechi zetu zilizobaki tunakuwa vizuri na kupunguza makosa katika eneo hilo,” alisema Kitambi.

Alisema wanapambana ili kupata mechi za kirafiki kabla ya kumalizika wiki hii ili ziwape mazoezi mazuri kuelekea mchezo wao dhidi ya Mbeya City.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliofanyika Novemba 4, mwaka jana kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, Namungo ililala kwa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City.

Namungo iko nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 32 baada ya kucheza michezo 25, imeshinda tisa, imetoka sare michezo mitano na kupoteza 11. Namungo iko nafasi ya nane ikiwa na pointi 32 ikifunga mabao 23 imefungwa 28.

Chanzo: Mwanaspoti