Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namungo yaililia Bodi ya Ligi Kuu

Namungo FC Window Wachezaji wa Namungo FC

Thu, 29 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya wenyeji Coastal Union na Namungo huenda ukaota mbawa kutokana na ratiba kwa wageni wa mchezo huo kuwa ngumu.

Iko hivi; Namungo ni wawakilishi wa Bara kwenye mashindano ya Mapinduzi yanayotarajia kuanza mapema wiki ijayo kwa kushirikisha timu 12, huku tano zikitoka Bara, tano Zanzibar na moja ya Burundi.

Wakati Namungo ikiwa na ratiba ya kucheza na Januari Mosi dhidi ya Coastal Union kwenye ratiba ya Mapinduzi inaonyesha Januari 2, itakuwa na kibarua dhidi ya Chipukizi.

Akizungumza kocha wa Namungo, Denis Kitambi alisema ni kweli ratiba kwao itakuwa ngumu hawataweza kucheza mechi mbili mfululizo ikiwa inafanyika bara na visiwani na sasa wamezungumza na Bodi ya Ligi ili waweze kuusogeza mchezo huo mbele.

“Tumefanya mazungumzo na Bodi ya Ligi kutokana na ugumu wa ratiba hiyo tunasubiri majibu yatakuwaje lakini ni ngumu kwetu kucheza mechi mbili ndani ya siku mbili bara na visiwani,” alisema.

“Kila mchezo ni muhimu kwa sababu yote ni mashindano ambayo kama timu tumethibitisha kushiriki hivyo tunatarajia kupata majibu mazuri kutoka kwao.”

Alipotafutwa Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi (TPLB), Karim Boimanda alisema hawezi kuzungumza lolote kuhusiana na hilo kwa sababu yupo nje ya kazi kwa mapumziko.

Chanzo: Mwanaspoti