Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namungo yaifuata Mlandege nusu fainali

Namungo Semi Final.jpeg Wachezaji wa Namungo FC

Fri, 6 Jan 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya Azam FC na Mlandege sasa ni zamu ya timu nyingine ya bara kutinga hatua ya nusu fainali na itakutana na Mlandege huku Azam FC ikimsubiri mshindi kati ya Yanga na Singida Big Stars.

Namungo ambayo ilikuwa kundi D na Chipukizi iliyomaliza na pointi mbili na Aigle Noir iliyofunga mkia kwa kupata pointi moja baada ya kuambulia sare dhidi ya Chipukizi.

Namungo ushindi wa leo umeifanya ikusanye pointi nne ilishinda mechi moja dhidi ya Aigle Noir bao likikwamishwa nyavuni na Hassan Kabunda dakika ya 62.

Kwenye mchezo huo ambao umemalizika kwa Aigle Noir wakicheza pungufu baada ya mchezaji wao mmoja kupewa kadi nyekundu haukuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote kucheza kwa kujilinda na kutumia mipira.

Kichuya ameibuka mchezaji bora wa mchezo huku mchezaji wa Aigle Noir Issah Ndikumana akiibuka mchezaji bora wa nidhamu.

Saa 2:15 Yanga atashuka dimbani kumenyana na Singida Big Stars tayari kusaka nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali.

Chanzo: Mwanaspoti