Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namungo yabanwa mbavu nyumbani

Namungo Vs KMC Majaliwa.jpeg Namungo wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya NBC

Sun, 2 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji wa kusini, Namungo FC wamepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara licha ya sare ya bila kufungana na KMC katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.

Namungo FC inafikisha pointi 11 katika mchezo wa tano na kupanda juu ya msimamo, ikizizidi pointi moja moja zote Simba na Yanga ambazo hata hivyo zina mechi moja moja mkononi.

Kwa upande wao, KMC wanafikisha pointi sita katika mchezo wa tano pia na kusogea nafasi ya tisa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live