Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namungo yaamua jambo kwa Simba, Yanga

Namungo Pioc Data Namungo yaamua jambo kwa Simba, Yanga

Thu, 1 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

LICHA ya kibarua kigumu kilichopo mbele yao kwenye mashindano ya kimataifa, kocha wa Namungo FC, Hemed Morocco amesema bado ana matumaini ya kuiongoza timu hiyo na kumaliza ndani ya nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara huku mbio za ubingwa akiwaachia Simba na Yanga.

Kocha huyo, alisema kuanza kurejea kikosini kwa baadhi ya wachezaji wake ambao walikuwa majeruhi, akiwamo beki wake wa kati, Aman Kyatta, ni habari njema kwao kutokana na kukabiliwa na mashindano mengi mbele yao.

“Hatupo sehemu nzuri, ni jukumu letu kama timu kupambana na kuhakikisha tunasogea nafasi za juu, hilo ni lengo letu kuu kwa sasa, kuhusu ubingwa hapana tumeachwa mbali na ni ngumu kusema tuna nafasi kwenye hilo,” alisema.

Aliongeza; “Ni muhimu kila mchezo kuupa uzito na kupambania pointi tatu, najua kwa kufanya hivyo tunaweza kufikia lengo.”

Namungo ambao mchezo wao ujao wa ligi watacheza dhidi ya Mbeya City, wapo nafasi ya 10 kwenye msimamo wakiwa na pointi 27 baada ya kucheza mechi 18, hivyo wana mechi 16 zilizobaki za kukamilisha msimu.

Kimahesabu wameachwa pointi 23 na vinara wa ligi hiyo Yanga wenye pointi 50 huku Wanajangwani wakiwa wamecheza mechi tano zaidi na pia wameachwa pointi 19 na Simba ambao wapo mbele yao kwa michezo miwili huku wakiwa pointi 46.

Related Simba Do or Die



Mkenya agundua mazito YangaAkizungumzia michezo miwili waliyopoteza ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco na Pyramids ya Misri, kocha huyo alisema wamepata somo hivyo ni matarajio yao kufanya vizuri mchezo ujao dhidi ya Nkana.

Namungo watakuwa nyumbani, Jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa kuikaribisha Nkana FC ya Zambia katika mchezo wa raundi ya tatu ya Kombe la Shirikisho Afrika.

“Kiukweli wenzetu wapo mbali na ukizingatia Namungo ni klabu changa ambayo taratibu ndio inakua, tumejifunza kwa wenzetu, naamini tulichopata kitatusaidia huko mbele, maandalizi yetu yapo vizuri na tuna imani kwamba tunaweza kufanya vizuri kwenye mchezo wetu ujao dhidi ya Nkana,” alisema kocha huyo.

Namungo na Nkana zimefungwa mechi zote.
Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz