Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namungo vitani Morocco leo

7834e43eae6aa478f1d0616e2dcb1edb Namungo vitani Morocco leo

Thu, 11 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TIMU ya Soka ya Namungo leo iko Casablanca, Morocco kucheza mechi ya kwanza ya kundi D katika hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Raja Casablanca ya huko.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Mohamed V.

Namungo kama timu ngeni katika michuano hiyo mikubwa imetinga hatua hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kuindosha Primeiro de Agosto ya Angola katika mchezo wa mwisho wa mtoano kwa jumla ya mabao 7-5.

Aidha, Raja ilitinga hatua hiyo baada ya kuiondoa US Monastir ya Tunisia kwa penalti 6-5 baada ya kila mmoja kushinda nyumbani kwake bao 1-0 na hivyo, kuwa na bao 1-1.

Wenyeji ni wazoefu katika michuano hiyo waliwahi kutwaa ubingwa wa kombe hilo mwaka 2018 lakini pia, 2019-2020 walifika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Imewahi kufika hatua za juu kwa vipindi tofauti na ni moja ya timu kubwa za Morocco zenye mafaniko makubwa kila msimu. Kwa sasa inaongoza ligi kwa pointi 19 katika michezo tisa ikiwa ni timu pekee haijapoteza mchezo wowote mpaka sasa.

Ukilinganisha timu hizo mbili kwa ubora kuanzia vikosi vyao Namungo iko chini ila katika mpira lolote linawezekana.

Kutokana na ubora wa timu hiyo ya Morocco Namungo inapaswa kuingia kwa tahadhari, nidhamu na mbinu ili kupata matokeo.

Huenda wenyeji wakawadharau kwasababu ni timu ndogo ila wao wakijipanga vizuri kwa kuwaheshimu wanaweza kuwashangaza.

Namungo kwenye ligi bado haijarudi katika kiwango chake, inashika nafasi ya tisa kwa pointi 27 katika michezo 18 pengine ni kwasababu nguvu zao kubwa wameziweka kimataifa.

Lakini mwenendo wa ligi ni tofauti na michuano hiyo mikubwa wanaweza kubadilika na kuwa watu wengine tofauti kwenye michuano hiyo mikubwa.

Wakipata ushindi au sare ugenini ni matokeo mazuri wanarudi kujipanga kwa ajili ya michezo mingine.

Ikiwa watafungwa bado watakuwa na nafasi ya kurudi kujisahihisha na kujipanga kwa michezo mingine ya kundi hilo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz