Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namungo tatizo lipo hapa

Namungo Ubingwa Namungo tatizo lipo hapa

Mon, 19 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Mara ya mwisho kwa Namungo kupata ushindi katika Ligi Kuu Bara ilikuwa Novemba 26 ilipoilaza Dodoma Jiji bao 1-0 na baada ya hapo imecheza michezo mitatu mfululizo ya ligi hiyo bila kupata matokeo mazuri na kocha wa timu hiyo, Denis Kitambi ameweka wazi kinachoiponza.

Kitambi aliyetangazwa hivi karibuni kukaimu ukocha mkuu, alisema tatizo kubwa kwa kikosi hicho ni kukosekana fundi wa mpira wa kuunganisha safu ya kiungo na ushambuliaji.

Kauli ya Kitambi imekuja baada ya juzi timu hiyo kulazimisha sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar ugenini, licha ya wenyeji wao kucheza kwa dakika 60 wakiwa pungufu baada ya straika wao, Charles Ilanfya kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea madhambi, Abdulmalick Zacharia.

“Ugumu ulianzia baada ya kadi nyekundu kwani wapinzani wetu walijitoa zaidi tofauti na mwanzo, japo tunapaswa kujilaumu kwani tuliwapa nafasi ya kututangulia na kufanya mchezo kutuwia vigumu.”

Kitambi aliongeza licha ya muda mchache aliokuwa na timu hiyo ila ameona upungufu kwenye utengenezaji wa nafasi.

“Unaweza ukalaumu washambuliaji lakini ukiangalia hakuna mchezaji mzuri anayeweza kuunganisha safu ya kiungo na ushambuliaji vizuri, ndio maana hata nafasi ambazo tunatengeneza unaona ni chache mno,” alisema.

Kuhusu kuboresha kikosi hicho katika dirisha hili Kitambi alisema bado kuna muda wa kufanya hivyo ila kwa sasa anaendelea kuboresha maeneo yenye upungufu kabla ya kuletewa mastaa wapya ili kuongeza nguvu.

Huo ni mchezo wa pili kwa Kitambi tangu alipojiunga na kikosi hicho bila ya ushindi baada ya awali kufungwa na Yanga mabao 2-0 Desemba 7.

Chanzo: Mwanaspoti