Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namungo mguu sawa kwa Agosto

F7c3855ae6095b64debeedeafd40146f.jpeg Namungo mguu sawa kwa Agosto

Fri, 12 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KIKOSI cha Namungo FC leo kinatarajiwa kuanza safari ya Angola kuwafuata wenyeji wao Primeiro de Agosto watakaocheza nao mechi ya hatua ya 32 ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika keshokutwa.

Katika mchezo huo Namungo inahitaji ushindi ili kurahisisha kazi katika mechi ya marudiano nyumbani wiki mbili zijazo.

Mtendaji mpya wa Namungo, Omar Kaya aliliambia gazeti hili jana kuwa mipango yote ya safari iko tayari.

“Maandalizi yote kwa maana ya benchi la ufundi yamekamilika na mategemeo yetu kesho (leo) tuanze safari kujipanga kwa mchezo ambao umepangwa kuchezwa Jumapili ya wiki hii (keshokutwa),” alisema.

Kaya alisema malengo yao ni kwenda kuibuka na ushindi huku wakiomba kuungwa mkono na Watanzania wote bila kujali imani ya timu zao kwani kufanya vyema kwa Namungo ni faida kwa nchi.

“Sioni sababu ya Watanzania kuanza kujitenga na kuiacha Namungo ikipambana peke yake au kuwaachia watu wa ukanda wa Kusini, ni wakati wa kuweka nguvu pamoja kwakuwa ukiwa nje ya nchi wapinzani wanasema wanacheza na Watanzania,” alisema.

Namungo kama itafanya vizuri kwenye mchezo huo na ule wa marudiano itatinga hatua ya makundi ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya klabu Afrika.

Chanzo: habarileo.co.tz