Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namungo mambo magumu

8657858df1b9cd0212ddfa72cb0b8d9e.png Namungo mambo magumu

Mon, 10 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TIMU ya Namungo FC kutoka Lindi imeshindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani wa Majaliwa, baada ya kulazimishwa suluhu na KMC mchezo wa kiporo wa Ligi Kuu Tanzania Bara mzunguko wa pili jana.

Namungo ambao licha ya kuliandama lango la KMC kwa muda mrefu, kukosekana kwa utulivu kwa washambuliaji wake, Steven Sey kuliwanyima bao dakika ya 10 na Reliant Lusajo pia alikosa bao la wazi dakika ya 79 na 85.

Matokeo hayo yanaifanya Namungo kufikisha pointi 32 na kubakia katika nafasi ya 12 baada ya kushuka uwanjani mara 24 wakiwa nyuma ya Coastal Union ambao wanashika nafasi ya 11 wakiwa na pointi 33.

Nao wapinzani wao katika mchezo huo KMC wameendelea kubaki katika nafasi ya tano wakiwa na pointi 41 baada ya kushuka uwanjani mara 28 na kuendelea kusubiri nyuma ya Biashara United ambayo inakamata nafasi ya nne ikiwa na pointi 44.

Wakati huo huo, Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea tena kesho, ambapo katika Uwanja wa Mkapa, bingwa mtetezi wa ligi hiyo, Simba ataikaribisha Coastal Union kutoka Tanga, wakati katika Uwanja wa Mwadui Complex, wenyeji Mwadui watawakaribisha Kagera Sugar kutoka Bukoba.

Chanzo: www.habarileo.co.tz