Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namungo kung’oa wanne dirisha dogo

Namungo FC Window Wachezaji wa Namungo FC

Wed, 14 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Katibu wa Namungo FC, Ally Selemani, amesema katika kuhakikisha kikosi chao kinakuwa imara mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara watalazimika kuachana na baadhi ya wachezaji ili kuongeza nguvu mpya.

Alisema hadi sasa kabla ya ripoti ya mwalimu kuwafikia kama uongozi wamedhamiria kuongeza wachezaji wanne katika dirisha dogo litakalofunguliwa Desemba 15.

Selemani alisema mipango ya wachezaji watakaoongezwa tayari inaenda vizuri kwa kushirikiana na kocha kujua wapi panatakiwa kuimarishwa zaidi.

“Tutaongeza wachezaji wanne yaani washambuliaji wawili, beki mmoja na kiungo mmoja kwa sababu tunatakiwa kuwa na kikosi imara kila eneo hasa baada ya mzunguko wa kwanza kuonekana kuna mahali tumeyumba.

“Kocha anamalizia ripoti yake ndani ya siku hizi mbili uongozi utakuwa umeshaipokea na kuona wapi amependekeza na kina nani wanahitajika lakini kama uongozi tumeona wachezaji wasiopungua wanne watahitajika,” alisema Suleimani.

Namungo imemaliza mzunguko wa kwanza ikiwa nafasi ya tisa ikivuna alama 18 baada ya kushinda michezo mitano. sare tatu na kupoteza michezo saba.

Mshambuliaji Reliants Lusajo, mwenye mabao sita ndiye tegemeo la timu na muda mrefu hajafumania nyavu hivyo inawezekana ni moja ya sababu ya uongozi kuona namna ya kuongeza washambuliaji wawili kwenye eneo hilo.

Wikiendi hii Namungo itakuwa kwenye Uwanja wa Manungu kukipiga na Mtibwa Sugar.

Chanzo: Mwanaspoti