Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namungo aimhofii yeyote kimataifa

80774491096e5bdaafa62004208348d2 Namungo aimhofii yeyote kimataifa

Mon, 1 Mar 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MWENYEKITI wa Namungo Hassan Zidadu amesema Namungo haimuogopi kigogo yeyote katika kundi walilopangwa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika bali wanajipanga kufanya vizuri.

Namungo ilifuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo baada ya kuiondoa Primeiro de Agosto ya Angola kwa jumla ya mabao 7-5, ikishinda mchezo wa kwanza 6-2 na kufungwa mchezo wa pili 3-1.

Akizungumza Dar es Salaam jana Zidadu alisema wanashukuru kwa hatua waliyofikia na wanachojivunia ni ubora wa kikosi chao na kuwataka watanzania kuiamini timu yao.

“Watanzania wasiogope kwamba tunaenda eneo ambalo ni gumu labda tunakutana na vigogo wanaweza kutushusha kwa kutuona ni wadogo na sisi tukatumia fursa ya kuwafunga kwa kutudharau,”alisema.

Zidadu alisema hatua waliyofikia wanashukuru na wanaamini imetokana na dua za watanzania na kuwaomba kuendelea kuwaombea mema wafanye vizuri zaidi.

Alisema hatua waliyofikia wapo ambao hawakuwahi kufika na wao wakiwa wageni wamefanikiwa.

Kiongozi huyo alisema mashindano hayo wamejifunza mengi kwani kuna changamoto nyingi zimetokea ikiwemo kutumia nguvu kubwa kimataifa huku upande wa ligi juhudi zikipungua.

Alisema wamekuwa hawafanyi vizuri katika ligi sio kwa kupenda bali ni kutokana na majukumu waliyokuwa nayo ya kimataifa lakini sasa anaamini watarudi katika ubora wao kwa kuwa wanaendelea kujipanga kujiweka sawa.

Wakati huo huo, Kocha Mkuu wa kikosi hicho Hemed Morocco alisema muhimu ni kujipanga wakifanya marekebisho watafanya vizuri hatua inayofuata.

Namungo ipo kundi D lenye timu za Raja Casablanca, Nkana ya Zambia na Pyramid ya Misri.

Timu hiyo inatarajiwa kuanza ugenini mechi yake ya kwanza ya makundi dhidi ya Raja Machi 10, mwaka huu.

Chanzo: habarileo.co.tz