Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namungo, Prisons hakuna mbabe Ilulu

Namungo Vs Prisons Mchezo wa Namungo na Prisons umemalizika kwa sare ya magoli 3-3

Sat, 21 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Namungo FC wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 3-3 na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.

Mabao ya Namungo FC yamefungwa na Haruna Shamte dakika ya tano, Nurdine Chona aliyejifunga dakika ya 65 na Lucas Kikoti dakika ya 86, wakati ya Prisons yamefungwa na Ezekia Mwashilindi dakika ya nane, Jumanne Elfadhili kwa penalti dakika ya 56 na Moses Kitundu dakika ya 77.

Kwa matokeo hayo, Namungo wanafikisha pointi 37 na kuendelea kushika nafasi ya tatu, wakati Tanzania Prisons wanafikisha pointi 24 na kusogea kwa nafasi moja juu hadi ya 14 baada ya wote kucheza mechi 25.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live