Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namungo, KMC hakuna mbabe

Namungo Vs KMC (600 X 724) Namungo, KMC hakuna mbabe

Sat, 23 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Namungo imeshindwa kutamba katika uwanja wa Ilulu mkoani Lindi baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya KMC.

KMC walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Charles Ilanfya dakika ya 30, baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Matteo Anthony iliyomshinda golikipa wa Namungo Jonathan Nahimana.

Namungo ilifanya mashambulizi na kurejesha bao hilo dakika ya 44 kwa mkwaju wa penati kupitia kwa winga wa timu hiyo Shiza Kichuya baada ya mlinzi wa KMC Kenny Mwambungu kumfanyia madhambi mshambuliaji Obrey Chirwa kwenye eneo la hatari.

Matokeo hayo yanaendelea kuwa mabaya kwa KMC ambayo katika michezo minne imeshindwa kupata ushindi msimu huu, huku ikifanikiwa kufunga bao moja na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara tano.

Timu hiyo kutoka Manispaa ya Kinondoni ilianza Ligi Kuu Bara kwa kichapo cha mabao 2-0, kutoka kwa Polisi Tanzania, wakalazimishwa suluhu ya 0-0 na Coastal Union, wakapoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Yanga kisha sare ya kufungana bao 1-1 na Namungo.

Kwa upande wa Namungo wao walianza kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Geita Gold, wakalazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Kagera Sugar kisha wakapoteza kwa bao 1-0 kutoka kwa matajiri wa Jiji la Dar es Salaam Azam FC.

Namungo inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi tano wakati KMC iko nafasi ya 13, ikiwa na alama mbili baada ya timu zote kucheza michezo minne. Advertisement

Chanzo: www.tanzaniaweb.live