Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namungo, Biashara hakuna mbabe Ilulu

04e92741e99a6f6dfd31656334b45e01.jpeg Winga wa Namungo, Shiza Kichuya akijaribu kumtoka mchezaji wa Biashara

Fri, 31 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Namungo FC, jana imeshindwa kuutumia vyema Uwanja wake wa nyumbani wa Ilulu, mkoani Lindi baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya vibonde Biashara United kutoka mkoani Mara.

Namungo ilikuwa ya kwanza kuandika bao dakika ya 10 mfungaji akiwa Reliant Lusajo aliyefunga kwa kichwa akitumia vema mpira wa krosi wa Hashim Manyanya.

Bao hilo liliiamsha Biashara United ambayo ilianza kuliandama lango la Namungo kwa kufanya mashambulizi ya nguvu na katika dakika ya 38, walisawazisha kupitia kwa Denis Nkane, aliyefunga kwa kichwa akimalizia pasi ya Atupele Green.

Hadi timu hizo zinaenda mapumziko matokeo yalikuwa 1-1, kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikifanya mashambulizi ya kushtukiza lakini ubora wa walinda mlango ilikuwa vikwazo hivyo hadi dakika 90 zinatamatika timu hizo ziligawana pointi.

Matokeo hayo yanaifanya Namungo kufikisha pointi 13 na kusalia katika nafasi ya nane baada ya kushuka uwanjani mara 11 wakati BiasharaUnited imeendelea kusalia mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi tisa sawa na Kagera Sugar, wakipishana mabao ya kufunga na kufungwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live