Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namba zinazombeba Messi Ballon d'Or 2023

Lionel Messi Ballon D'OR 2023 Namba zinazombeba Messi Ballon d'Or 2023

Sun, 22 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Supastaa Lionel Messi anapewa nafasi kubwa ya kushinda Ballon d’Or 2023, huku kukidaiwa kuwapo na taarifa tayari zinazothibitisha kwamba mwamba huyo wa Argentina ananyakua tuzo hiyo kwa mara ya nane katika maisha yake.

Hata hivyo, maswali yamekuwa mengi kuhusu Messi, je ni kweli anastahili kubeba tuzo hiyo?

Kuna takwimu za kibabe kabisa zinazothibitisha nafasi hiyo kubwa kwa Messi kushinda.

Kwa kifupi tu, Messi tayari ameshashinda Ballon d’Or mara saba katika maisha yake ya soka na amekuwa namba mbili mara tano tofauti.

Wakati sasa akiachana na soka la Ulaya na kutimkia zake huko Inter Miami ya Marekani, Messi, 36, bado amekuwa akijadiliwa kwenye tuzo hiyo kwa kile alichofanya uwanjani.

Ikumbukwe tu msimu wa 2022-23 ulivuruga sana mashabiki wa soka kwa sababu fainali za Kombe la Dunia zilifanyika katikati ya msimu ikiwa ni mara ya kwanza kwenye historia.

Kiwango cha Messi kwenye fainali za Kombe la Dunia pekee yake kilitosha kumfanya ajadiliwe kwenye Ballon d’Or, kwa sababu mwanzo mwisho alitoa mchango mkubwa katika kuipa Argentina ubingwa wa taji hilo kubwa kabisa duniani kwa upande wa timu za taifa.

Hata hivyo, hiyo haina maana kwamba Messi hakuwa kwenye ubora wa kutosha kwenye mikikimikiki ya ligi za ndani pia. Sambamba na taji la Kombe la Dunia, Messi alishinda pia Ligue 1 na Trophee des Champions.

Upinzani mkali unaomkabili Messi kwenye tuzo hizo za Ballon d’Or kwa mwaka huu ni straika wa Manchester City, Erling Haaland ambaye alifunga mabao 52 na kuisaidia timu yake kushinda mataji matatu, Ligi Kuu England, Kombe la Ligi na Kombe la FA msimu uliopita.

Ingekuwa msimu mwingine, Haaland angekuwa na nafasi kubwa ya kushinda tuzo hiyo, lakini bahati mbaya kwake imetokea kipindi ambacho anashindana na fundi wa mpira.

Hzvi hapa takwimu 12 matata zinazompa Messi nafasi kubwa ya kushinda Ballon d’Or 2023.

1. Messi ameshinda mataji matatu msimu wa 2022-23, akishinda Kombe la Dunia, Ligue 1 na Trophee des Champions.

2. Kwa klabu na nchi yake, Messi alichangia mabao 67 katika kipindi cha upigaji kura za Ballon d’Or. Hiyo ina maana amemzidi Haaland bao moja katika kipindi hicho.

3. Messi alichaguliwa Mchezaji Bora wa Mechi mara tano katika mechi saba za Argentina ilizocheza kwenye Kombe la Dunia 2022. Hakuna mchezaji mwingine aliyewahi kufanya hivyo.

4. Messi amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga kwenye hatua ya makundi, raundi ya 16 bora, robo fainali, nusu fainali na fainali yenyewe kwenye fainali moja za Kombe la Dunia.

5. Messi alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Kombe la Dunia katika fainali hizo za Qatar na hivyo kuwa mchezaji wa kwanza kushinda mara mbili (2014 na 2022).

6. Ni Kylian Mbappe pekee (mabao manane, 2022) na Ronaldo (mabao manane, 2002) ndiyo waliofunga mabao mengi kwenye fainali moja za Kombe la Dunia kumzidi Messi (mabao saba, 2022) katika fainali 12 zilizopita, zikianzia 1974.

7. Messi alikuwa mchezaji bora kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2022-23 kwa mujibu wa takwimu za WhoScored. Staa huyo alikuwa na wastani wa 7.86 ikiwa ni kubwa kuzidi wote.

8. Katika soka la ndani, Messi alipiga mashuti 197 katika msimu wa 2022-23. Katika Ligi Kuu tano bora za Ulaya, staa wa Manchester United, Bruno Fernandes peke yake ndiye aliyepiga mashuti mengi kumzidi, 219.

9. Messi alitengeneza mabao 35 akiwa na PSG, ikiwa ni idadi kubwa zaidi ya kuhusika kwenye mabao kuliko wachezaji wengine wote huko Ulaya katika msimu wa 2022-23.

10. Messi alifanya majaribio mara 102 ya kuvuka wapinzani akiwa na mpira na kufanikiwa kwa asilimia 55.4. Ni staa wa Real Madrid, Vinicius Junior ndiye pekee alifanya majaribio mengi kumsizi Messi kwenye msimu wa 2022-23, alipofanya hivyo mara 112.

11. Hakuna mchezaji kwenye Ligi Kuu tano bora za Ulaya aliasisti mabao mengi kumzidi Messi msimu wa 2022-23. Kwenye Ligue 1, Messi aliasisti mara 16, kama ambavyo alifanya Antoine Griezmann na Kevin De Bruyne. Messi ana wastani mzuri wa kuasisti.

12. Katika michuano yote, wastani wa mchango wake kwa kila bao ni dakika 89 alipokuwa na kikosi cha PSG, ambapo alifunga mabao 21 na kuasisti 20 kwa 2022-2023.

Chanzo: Mwanaspoti