Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namba zambeba Saido Yanga

Kikosi Cha Yanga .png Namba zambeba Saido Yanga

Thu, 15 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MRUNDI wa Yanga, Said Ntibanzokiza namba zinambeba. Mwanaspoti limefanya uchambuzi wa umuhimu wa Saido licha ya kucheza mechi chache na dakika chache tangu ajiunge na kikosi hicho,aliposajiliwa dirisha dogo.

DAKIKA 280

Kila dakika 46 za kwanza anazokuwepo uwanjani anahusika na bao, akiwa amecheza jumla ya dakika 280 tangu aanze kuichezea timu hiyo, msimu huu.

ASISTI 4

Saido mwenye miaka 33, hana mpinzani katika kikosi cha kwanza cha Yanga, licha ya kucheza dakika chache (280),ndiye mchezaji aliyefanya mambo makubwa katika mechi 3 ametoa pasi za mabao 4 dhidi ya Dodoma Mji dakika ya 45, Yanga ikishinda mabao 3-1.

Saido katika mechi na Ihefu, katika ushindi wa mabao 3-0 ulioipata Yanga alihusika na mabao mawili akitoa pasi za mabao, mechi nyingi ambayo alitoa pasi ni dhidi ya KMC, timu hizo zikitoshana nguvu.

MABAO 2

Katika dakika chache alizocheza (280) hajaishia kuisaidia timu hiyo kutoa pasi za mabao, bali amefunga mabao mawili dhidi ya Dodoma Mji na Prisons

POINTI 7

Nyota huyo ameisaidia Yanga kuvuna pointi saba kwenye michezo mitatu ya mwisho kwake kuichezea timu hiyo ya Wananchi, hiyo inaonyesha jinsi ambavyo amekuwa na mchango mkubwa.

Kwa namna ambavyo amekuwa akijituma ni wazi kuwa Saido ndiye mchezaji hatari zaidi kwa sasa kwenye safu ya ushambuliaji ya timu hiyo licha ya uwepo wa Yacouba Sogne na Fiston Abdoulrazak.

JEZI 60

Pamoja na kwamba amekuwa akipenda kuvaa jezi namba 10, Saido hakutaka mvutano ndio maana aliamua kumwachia Yacouba jezi hiyo na kuamua kuvaa jezi namba 60.

Kocha Juma Mwambusi amemuelezea kama miongoni mwa wachezaji wanaoweza kubadili taswira ya Yanga kwenye mechi zilizosalia kwenye Ligi.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz