Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namba za mzize zinatisha Yanga

Mzize Nabi Pc Namba za mzize zinatisha Yanga

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji kinda wa Klabu ya Yanga, Clement Walid Mzize amekuwa na mchango mkubwa kwenye timu yake tangu apandishwe daraja na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Nasreddine Nabi mwanzoni mwa msimu wa 2022/23.

Mzize ambaye alipandishwa kutoka timu ya vijana akiwa mfungaji Bora wa Ligi ya Under 20 msimu huo, ameisaidia Yanga hasa kwenye nyakati ngumu.

Walid Mzize katika Ligi Kuu Tanzania bara tangu apandishwe timu ya wakubwa ya Young Africans amekuwa mchezaji wa tatu ndani ya kikosi hicho cha Wananchi kuhusika katika mabao mengi zaidi.

Tangu msimu uliopita, Mzize amecheza mechi 40 amehusika katika mabao 16 akiwa amefunga mabao 9 na assists 7.

Tangu ulipoanza msimu uliopita ni wachezaji watatu pekee kwa Young Africans ndio wamehusika katika mabao zaidi ya 15 katika ligi.

Stephane Aziz Ki ndiye anaongoza akiwa amehusika kwenye mabao 34, amefunga mabao 23 na assists 11. Fiston Mayele amehusika katika mabao 20 akiwa amefunga mabao 17 na assists 3.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: