Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namba za Alaba zinatisha Madrid

David Alaba Madrid Mlinzi wa Real Madrid, David Alaba

Fri, 13 Jan 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Takwimu za David Alaba zimeonyesha kiwango chake kimeshuka kwa mara ya kwanza kwa mujibu wa ripoti za data zilizotolewa Hispania.

Real Madrid ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa La Liga kwa tofauti ya pointi tatu dhidi ya Barcelona baada ya ushindi wa bao 1-0 iliopuata ilipomenyana na Atletico Madrid wikiendi iliyopita.

Imeelezwa safu ya ulinzi ya Real Madrid kwa sasa imetetereka baada ya Thibaut Courtois kupata majeraha huku Antonio Rudiger akionekana bado hajafiti kwa asilimia 100 chini ya Carlo Ancelotti.

Alaba alicheza sambamba na Eder Militao katika safu ya ulinzi msimu uliopita, lakini kiwango cha beki huyo wa kimataifa wa Austria kimeshuka kwa asilimia kubwa.

Takwimu zinaonyesha Alaba ameshuka kwa thamani ya 0.100, hiyo inaamanisha alizuia mabao kwenye safu ya ulinzi, katika mechi 10 tu tofauti ilivyokuwa msimu uliopita. Msimu uliopita mchango ake katika safu ya ulinzi ilikuwa thamani ya 0.275 tofauti na takwimu zake zilivyoripotiwa msimu huu. Vilevile takwimu zimeonyesha kiwango cha Alaba kimeshuka na kufikia 00.6 kutoka 00.12 alivyocheza msimu uliopita.

Madrid ilipokea kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Villarreal wikiendi iliyopita, safu yao ya ulinzi ikipondwa na wachambuzi wa soka La Liga, huku Alaba akiendelea kuboronga.

Kwenye mtanange huo Alaba alisababisha penalti baada ya kuunawa mpira, Genaro Moreno akiwaua Madrid kwa mkwaju wa penalti dakika za mwisho.

Aidha Alaba atakuwa nje ya dimba kwa wiki tatu kadhaa baada ya kuumia taarifa hiyo imethibithishwa na Madrid. Nafasi ya Alaba itachukuliwa na Rudiger kwenye safu ya ulinzi na atacheza sambamba na Militao.

Chanzo: Mwanaspoti