Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Najisikia fahari kuwa sehemu ya Dabi kubwa Afrika" Nabi

Nabi Pc Data Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi

Fri, 24 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa Kikosi cha Dar Young Afrika,Nasreddine Nabi, amesema anajisikia fahari kuwa mmoja wa Makocha wanaoshiriki moja ya Dabi kubwa barani Afrika,Dabi ya Simba na Yanga.

Kocha huyo wa Yanga amesema hayo wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari kuelekea mtanange huo Septemba 25, katika uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar.

"Hii ni dabi yangu ya tatu tangu nije Yanga, hii si dabi ya kawaida ni kama fainali kwa kuwa ina kikombe kwa hiyo ni lazima mshindi apatikane" amesema Kocha Nabi

"kuna idadi kubwa ya watu wanaoifatilia Dabi hii kutoka kila pembe ya Afrika, na kuwa miongoni mwa makocha sio kitu kidogo"

Tangu atue kunako kikosi cha Wanajangwani, hii inakwenda kuwa mechi yake ya tatu kocha huyo dhidi ya Mnyama Simba SC, mechi ya kwanza walikutana katika Ligi mzunguko wa pili na akaibuka na ushindi wa goli 1-0 likiwekwa wavuni na kiungo Zawadi Mauya.

Mechi ya Pili ni katika Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam ambako alipoteza kwa goli 1-0 goli likifungwa na Taddeo Lwanga.

Hivyo ameahidi kuhakikisha anafanya vyema ili angalau waibuke na ushindi katika mchezo huo wa Ngao ya Hisani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live