Najiat Idrisa ni jina ambalo halisauliki masikioni mwa Ivory Coast akiwa na timu ya taifa ya wanawake 'Twiga Stars' na CBE ya Ethiopia akiwa na timu yake ya JKT Queens hii ni maada ya kuwapa kilio kwenye matokeo ya mwisho kuamua nafasi tofauti.
Watanzania wanamfahamu zaidi baada ya kuwapa nafasi ya kutinga hatua inayofuata kuwania tiketi ya kushiriki Wafcon 2024 wakiwaachia kilio mastaa wa Ivory Coast ambao walitumia dakika 90 bora bila ya kuambulia bao lolote.
Wakati wa Ivory Coast wakiwa na maumivu hayo pia alifanya hivyo dhidi ya CEB ya Ethiopia kwenye mashindano ya CECAFA akiisaidia timu yake JKT Queens kutwaa taji.
Mwanaspoti limepata nafasi ya kufanya mazungumzo na kipa huyo ambaye amefunguka mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na rekodi yake nzuri kwenye upanguaji wa penati kwenye mechi muhimu.
CECAFA SASA WAFCON
Ubora wa kupangua penati mbili dhidi ya Ivory Coast umemfanya azungumziwe sana na wadau wa soka nchini hii ni kutokana na kumshukudia lakini mwenyewe anafunguka kuwa sio mara yake ya kwanza kufanya hivyo.
"Nafikiri watanzania wamenitazama kwenye mashindano haya na kubaini ubora wangu lakini sio mara yangu ya kwanza kusaidia timu nikiwa langoni nakumbuka mara ya mwizo ni kwenye mashindano ya CECAFA;
"Sio mala ya kwanza nimefanya ivyo Uganda pia kwenye Kombe lao la ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati kwa Wanawake (CECAFA) baada ya dakika 90 mchezo kumalizika kwa suluhu tuliingia kwenye hatua ya matuta nilipangua moja na kuisaidia timu yangu kuibuka mabingwa kwa ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya CBE ya Ethiopia Uwanja wa Kituo cha Ufundi cha FUFA, Njeru mjini Kampala nchini Uganda." anasema
SIO KUDAKA TU HADI KUFUNGA
Wakati ushujaa wake ukiendelea kujadiliwa na wadau wa soka baada ya kudaka penati mbili kati ya tano walizokuwa wanapigiana na Ivory Coast kipa Najiat amefunguka kuwa mbali na nafasi ya kipa yeye ni mshambuliaji.
"Nimekaa langoni nimefanikiwa kuokoa mikwaju ya penati kila mtanzania amefurahia lakini ninachoweza kusema hata nikipewa dakika 90 leo hii nicheze eneo la ushambuliaji naweza kufanya hivyo na matokeo yakapatikana;
"Tangu nimeanza kucheza mpira nilikuwa nacheza eneo la ushambuliaji lakini mara baada ya kujiunga na kituo cha Makongo chini ya Oscar Milambo nilibadili nafasi na kukaa langoni." anasema.
Najiat anasema Oscar ndiye aliyembadili nafasi lakinbi hiyo haimuondolei ubora wake katika eneo la kushambulia kwani bado anapenda kucheza nafasi hiyo na kuna muda akiwa mazoezini anafanyia kazi eneo hilo pia.
UTANI ULIVYOMVUNJA MGUU
Utani katika kazi na kwenye maisha ya kawaida huwa unafanyika sana lakini sio kila utani unakuwa mzuri kuna wa kuumiza na wa kuchekesha kama anavyothibitisha Najiat.
"Nakumbuka tukiwa timu ya taifa kujiandaa na mchezo kabla ya mazoezi utani utani nikaruka juu kupiga kichwa mpira nilipo tua chini goti likaumia na nilichukulia kama utani lakini baada ya vipimo nilibainika kuvunjiaka;
"Tukio hilo liliniweka nje ya uwanja kwa miaka miwili sitakaa nikasahau na hilo ndio tukio langu la kizembe nililowahi kufanya uwanjani na kunisababishia maumivu makali." anasema kipa huyo.
AMTAJA MABANZA
Kila myu na mbabe wake hivyo ndio unaweza kusema hii ni baada ya Najiat kumtaja Ester Mabanza anaekipiga Fountain Gate Princess kuwa ndiye mpigaji penati mzuri anayemkubali.
"Wengi ni wazuri kwenye suala la upigaji lakini Mabanza ni fundi zaidi hajawahi kukosa tangu nimemfahamu kwenye maisha yangu ya soka kuna wengine wengi ila chaguo langu ni hilo." anasema.
NI MJESHI
Licha ya kucheza soka tayari ni muajiliwa kwani ni mwanajeshi hii ni baada ya kwenda kozi amekili kuwa ni moja ya ndoto yake tangu alipokuwa anakua.
"Kabla ya maisha ya soka ndoto yangu ilikuwa ni kuwa mwanajeshi nashukuru Mungu imetimia pia sasa napambania maisha ya soka ikitokea nikaamua kukaa mbembeni nitarudi kwenye majukumu mengine;
"Kuna maisha baada ya mpira japo napenda kucheza lakini naamini katika kazi ambayo nilikuwa naipenda na kuipa kipaumbele nashukuru wazazi wangu walinisapoti kwenye kila kitu nilichokuwa natamani kukifanya." anasema kipa huyo aliyetokea Evergreen sasa anakipiga JKT Queens.
ALIYEVUNJIKA KISA SOKA AMPA ULAJI
Maisha ni kitendawili anayekitegua ni binadamu mwenyewe wakati mjomba mtu ambaye ndiye alikuwa anamshawishi kuingia kwenye soko kupata ulemavu na kuacha soka unambiwa huyohuyo ndiye aliyemsimamia Najiat kuhakikisha anatimiza ndoto yake.
"Nakumbuka kipindi naanza kucheza soka nikiwa na miaka 11 familia yangu hasa mlezi wangu ambaye ni bibi yangu alikuwa hataji kabisa kusikia hilo jamboo hii ni kutokana na mtoto wake amaye mimi ni mjomba angu kuvunjika;
"Bibi yangu ndio alikua ataki hata kusikia na kipindi hicho nilikua bado Mkoani na shule ya Makongo walikua wananitaka nikasome pale huku nacheza luhusa ilikua ngumu mno kutokana na changamoto iliyowahi kumkuta mjomba angu;
"Lakini huwezi amini mjomba yangu Abdulmalik ndiye aliyesimama kidete kumjenga bibi kisaikolojia kumuaminisha kuwa changamoto iliyomkuta yeye haiwezi kunizuia kucheza alimwambia bibi yangu kua ajalie haina kinga anaweza baki hapa na akumia kwa kitu chochote tofauti na mpira na kumuomba aniache nije Dar es Salaam kusoma na kucheza mpira." anasema na kuongeza.
"Ndipo ruhusa yangu ikatoka kwa moyo mkunjufu huku nikiombewa mema katika kuhakikisha natimiza ndoto zangu Mjomba angu ndiye alikuwa mtu sahihi kwa kunisapoti akianza kunihudumia klwa kuninunulia vifaa vya micheza hadi sasa." anasema.
KISA SOKA MAMA PRESHA JUU
Sio wazazi wote licha ya kuwaruhusu watoto wao kucheza soka wanauwezo wa kuwatazama wanapocheza wengi wao wanawatakia heli kabla ya mchezo na baada ya matokeo kupiga simu kujua ilikuwaje bila ya kutazama hii ni kujiepusha na changamoto za matukio ya uwanjani.
"Msimu wa 2017 nakumbuka kulikuwa na mechi ya kirafiki ya timu ya taifa na Burundi ndio ilikuwa siku ya kwanza mama yangu kufuatilia mchezo siku hilo nilifanyiwa madhambi mama yangu alipata presha licha ya kufurahia kuniona nikishindana mara baada ya mchezo kuisha;
"Wazazi wa kike ni Mungu wetu wa pili hakuna ambaye anafurahia mtoto wake akifanyiwa kitu kibaya lakini tuklio hilo halikuwa kubwa sana ila mama tena akapata presha iliyomfanya adumu nayo hadi kifo kilipomfika tukio hilo linaniumiza sana." anasema Najiat ambaye alicheza mechi 18 msimu ulioisha na timu yake kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi.
NAMBA ZA MATUKIO
Kwenye maisha kila mwanadamu anakumbukizi ya siku ya kuzaliwa, mwezi wengine wanakumbukizi ya ndoa zao, matukio mabaya ya misipa inayowahusu watu wao muhimu kama alivyothibitisha kipa namba moja wa JKT Queens Najiat ambaye amekiti kuw ni mtoto wa kwanza kwenye familia ya watoto wawili.
"Nina namba tatu muhimu ambazo kila namba ina maana yake mwenye maisha yangu mbili ni tarehe yangu ya kuzaliwa nne ni mwezi na 18 ni siku ya maumivu kwenye maisha yangu hii ndio siku niliyompoteza rafiki yangu wa kweli mama yangu." anasema Najiat ambaye anavaa jezi namba 18 ikiwa ni kumuenzi mzazi wake huyo.