Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naj Razi awaingiza vitani vigogo Ulaya Arsenal

Naj Razi 630x402 Naj Razi

Sat, 4 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu za England Arsenal na Chelsea zinapamnbana na Real Madrid ya Hispania kumsajili mchezaji chipukizi wa Ireland, Naj Razi.

Razi ameonekana na klabu kubwa za Barani Ulaya baada ya kupangwa katika kikosi cha kwanza cha Shamrock Rovers FC msimu huu 2023/24.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka l7, amecheza mara tano kipindi hiki katika timu hiyo inayojulikana pia kama Hoops, ambayo juma hili itakuwa mwenyeji wa Sligo Rovers kwenye Uwanja wa Tallaght.

Na amekuwa na klabu hiyo tangu akiwa motto mdogo, alijiunga na shule ya timu hiyo akiwa na umri wa miaka saba.

Chipukizi huyo amewakilisha timu ya taifa ya Ireland ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 tangu mwaka 2022 na hadi sasa amecheza mechi 14 na kufunga mabao manne na kusaidia kupatikana kwa mabao manne.

Alianza katika mashindano ya umri chini ya miaka 17 ya Ireland ambayo ilitolewa katika Robo Fainali na Hispania baada ya kufanya vizuri katika hatua ya makundi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live