Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nahodha wa zamani wa Yanga afiwa na mkewe

95149 Nizar+pic Nahodha wa zamani wa Yanga afiwa na mkewe

Mon, 10 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

NYOTA na nahodha wa zamani wa Yanga, Nizar Khalfan, anayekipiga kwa sasa Rhino Rangers ya Tabora, iliyopo Ligi Daraja la Kwanza, amepata pigo kubwa baada ya kufiwa na mkewe mchana wa leo jijini Dar es Salaam. Nizar amepata msiba huo akiwa na chama lake jijini Tanga kwa ajili ya mechi yao dhidi Sahare All Stars ya Tanga inayochezwa jioni hii. Katibu wa Rhino Rangers, Rashid Kombo alisema Nizar alikuwa katika majukumu ya timu yao na hata katika mechi ya leo jioni dhidi ya Sahare alikuwa katika kikosi cha kwanza ila baada ya kupata taarifa hizo jambo hilo la kucheza likashindikana. "Nizar ilikuwa atumike katika kikosi cha kwanza leo lakini mchana ndio tukapata taarifa hizo za msiba kama uongozi tunatoa pole kwa wafiwa na watu wote walioguswa na msiba huo kama tulivyokuwa pamoja awali na mchezaji wetu kumpa ruhusa ya kurudi Dar, kushughulika na msiba. Tutaungana naye katika kipindi hiki kigumu," alisema Kombo. Mwanaspoti lilimtafuta Nizar, ambaye alionekana kutokuwa mahala penye utulivu na alionekana kuongea katika sauti ya chini akieleza kuwa msiba upo Mbagala hapa Dar es Salaam. "Msiba upo maeneo ya huko huko Mbagala na mazishi yatafanyika katika makaburi ya maeneo hayo," alieleza kwa ufupi Nizar ambaye amewahi kuzitumikia timu nyingi hapa nchini kama Yanga, Singida United na timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'. Msiba huo umekuja wiki chache tangu Nizar alipomtakia kila la heri mkewe kwenye siku yake ya kuzaliwa iliyokuwa Januari 21 mwaka huu.

Chanzo: mwananchi.co.tz