Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nahodha wa zamani wa Ghana kumlipa fidia mke wake wa zamani

 Nahodha Wa Zamani Wa Ghana Kumlipa Fidia Mke Wake Wa Zamani Nahodha wa zamani wa Ghana kumlipa fidia mke wake wa zamani

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Nahodha wa zamani wa Ghana Asamoah Gyan lazima alipe fidia kwa mke wake wa zamani baada ya mahakama kutoa uamuzi kuhusu kesi yao ya talaka na kuamua kuwa yeye ndiye baba mzazi wa watoto wao watatu.

Mahakama nchini Ghana ilimuamuru kijana huyo mwenye umri wa miaka 37 kumpa Gifty Gyan nyumba nchini Uingereza, nyumba mjini Accra, kituo cha mafuta na magari mawili.

Gyan na mke wake wa zamani wamekuwa kwenye vita vya kisheria kwa miaka mitatu, huku kesi ya talaka ya wanandoa hao ikitolewa kufuatia madai ya mwanasoka huyo kwa mke wake kutokuwa mwaminifu na madai yake kwamba watoto wao watatu huenda wasiwe wake.

Uchunguzi wa DNA ulikanusha madai yake. Siku ya Jumanne, mahakama iliamua kwamba mchezaji huyo wa zamani wa Udinese, Rennes na Sunderland lazima pia alipe cedis 25,000 za Ghana ($2,100, £1,729) kwa mwezi kwa ajili ya malezi ya watoto.

Ingawa wenzi hao walikuwa tayari wametengana, mahakama ilibatilisha ndoa hiyo kufuatia ombi lililojazwa na Asamoah Gyan.

Mahakama iliamua kwamba Gifty Gyan alikuwa ametoa mchango usio wa pesa katika ununuzi wa mali hizo kwa sababu ni yeye pekee aliyekuwa akiwalea watoto wao huku Gyan akifanya biashara yake.

Nyumba ya vyumba vinne huko Accra ilinunuliwa kwa ajili yake kabla ya ndoa yao ya 2013. Kabla ya kufunga ndoa rasmi miaka 10 iliyopita, wenzi hao walikuwa na watoto wawili.

Chanzo: Bbc